Wednesday, October 9, 2013

Vodacom yaendelea kuadhimisha wiki ya Huduma Kwa Wateja katika matawi yake nchi nzima

Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa Bi.Herieth Koka(kushoto)akimpatia mmoja wa wateja keki aliefika dukani hapo ikiwa ni ishara ya kuendelea kusherehekea na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimfanyia mahojiano Afisa Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Bi.Herieth Lwakatare,kuhusiana na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza akisalimiana na baadhi ya wateja waliofika kupata huduma mbalimbali Vodashop Mlimani City na kupata frusa ya kujumwika na Mkurugenzi huyo katika kusherehekea na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
Afisa Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Bi.Herieth Lwakatare(katikati)akipozi kwa picha na wafanyakazi wenzake.
Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Brigita Stephen akiwafafanulia jambo baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliotembelea makao makuu katika kusherehekea na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
Washindi wa zawadi ya huduma bora kwa wateja wa ndani waliochaguliwa na Idara ya Mahusianao na Mawasiliano na Idara ya Wateja wa Mikataba Zenobius Mlowe (kulia) kutoka idara ya manunuzi na Faraji Hiza(kulia) wa idara ya Huduma kwa Wateja wakiwa na tuzo zao katika picha ya pamoja na wasanii wa kike wa kizazi kipya mara baada ya kukabidhiwa tuzo zao katika hafla fupi iliyofanyika kwenye idara ya Mahusiano na Mawasiliano ya Vodacom Makao Makuu.
Meneja wa Mradi wa MWEI Bi.Grace Lyon kushoto aliesimama akiwa amepozi kwa picha na baadhi ya wasanii wakike wa kizazi kipya waliotembelea makao makuu ya Vodacom katika kusherehesha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wiki hii inaungana na dunia nzima katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo ambayo yalianza mnamo tarehe 7 yanaendelea mpaka tarehe 11 ya mwezi huu yakiambatana na shughuli mbalimbali ambazo zikifanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika jamii ambao wataendelea kujumuika pamoja na wateja wao sehemu mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika Makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City,jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza, alisema Vodacom inayofuraha kubwa sana kwa kuendelea kufurahishwa na kuungwa mkono na alitoa wito kwa watanzania kuendelea kutumia huduma ya M-PESA kwani ni sehemu ya maisha ya watanzania hivi sasa na kuwahakikishia kuwa kampuni yake itaendelea kutoa huduma bora na za uhakika za mawasiliano hapa nchini.

Katika ufunguzi huo, Meza kwa kushirikiana na wafanyakazi na baadhi ya wateja kwa pamoja walikata keki kuashiria kuanza kwa wiki hii ambapo wateja walipata kula pamoja. Vilevile zawadi mbalimbali ziligawiwa kama shukrani kwa kuunga mkono na kuendelea kutumia mtandao wa Vodacom.

Kama kampuni ushirikiano baina ya wateja na wafanyakazi ni jambo muhimu sana kwani huwa ni wakati muwafaka wa kubadilishana mawazo kujua nini wateja wanachokihitaji kiboreshwe na kupata majibu yaliyosahihi katika soko hili lenye ushindani."Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele siku zote sio tu katika kutoa huduma bora bali pia na kuwasikiliza wateja wanataka kitu gani.

Hivyo tungependa kuwaambia wateja wetu tunashukuru sana kwa kutuunga mkono kwa kipindi chote hicho na pia kuendelea kutumia huduma zetu," Meza alisema.

No comments:

Post a Comment