Saturday, September 7, 2013

RAIS SHEIN WA ZANZIBAR AFANYA UZINDUZI WA MADARASA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA MBWENI,ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,Dk.Haji Mwita,alipotembelea Dagfhalia ya Wanafuzi wa Chuo hicho kabla ya kuzindua madarasa ya Chuo hicho leo huko Mbweni nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,Dk.Haji Mwita,alipotembelea kuona vifaa mbali mbali vya kufundishia chuoni hapo alipofika kuzindua madarasa ya kusomea yaliyojenga kwa ufadhili wa Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,wakikata utepe kama ishara ya ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa ushauri wakati alipotembelea moja ya madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,huko mbweni baada ya kuyazindua rasmi leo,ambayo yamejengwa kwa ufadhili ya Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake,baada ya kuyazindua rasmi madarasa ya chuo hicho leo ,hapo chuoni Mbweni,Mkoa wa Mjini Mgharabi Nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Dk. Haji Mwita,baada ya kuyazindua Rasmi madarasa ya Kusomea,yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Oman,na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,akitoa salamu zake wakati wa sherehe za uzinduzi wa madarasa mapya ya kusomea katika Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,yaliyojengwa na Serikali ya Oman,na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,huko Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo,(kushoto) Waziri wa Afya Juma Duni Haji,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,(kulia).
Baadhi ya wananchi na viongozi walioalikwa katika sherehe za uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

No comments:

Post a Comment