Monday, September 23, 2013

NSSF YAIFUNGA NPF 2-1

TIMU ya soka ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mwishoni mwa wiki iliifunga iliyokuwa timu ya zamani ya shirika hilo, Shirika la Akiba ya Wafanyakazi (NPF), mabao 2-1 kwenye uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa kasi na dakika ya tano ya mchezo, NSSF walikosa bao kupitia kwa Ally Sham baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mahadhi Mohamoud.

NPF walijibu shambulizi hilo dakika ya 15 baada ya Juju Mtukuru kuwatoka mabeki wa NSSF na kuachia shuti kali lilodakwa na kipa Abubaka Soud.

Salehe Biboze aliipatia NSSF bao la kwanza dakika ya 55, kabla ya NPF kusawazisha dakika ya 67 kwa bao la Prosper Lyoba huku Khalid Jambia akipachika bao la yshindi dakika ya 79.

Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu alisema madhumuni ya mchezo huo, ni kuweka mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha afya zao.





Beki wa NSSF, Kitwana Kidatu (kulia) akiwania mpira huku akizomgwa na mshambuliaji wa NPF katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa TTC Chang'ombe jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 

 Mshambuliaji wa NSSF, Ally chuo akipata matibabu baada ya kuumia katika mchezo huo.
 Benchi la ufundi la timu ya NSSF
 Mshambuliaji wa timu ya NSSF, Ally Chuo (kushoto), akichuana na beki wa NPF wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Hekaheka.....
Wachezaji wa NSSF wakiwa mapumziko.
 Wachezaji wa NPF
Kikosi cha timu ya NSSF.
 Kikosi cha timu ya NPF
 Matibabu.
Waratibu wa mchezo huo, wakiongozwa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF,  Juma Kintu wa pili kushoto.

No comments:

Post a Comment