Tuesday, September 24, 2013

Mnara wa CN jijini Tornto, Canada

Mnara wa CN (The CN Tower) uliopo katikati ya jiji la Toronto, Canada, una urefu wa mita 553.33 ama futi 1,815.4, ambao hutumika kama mnara wa mawasiliano na pia kituo cha kuangalia mandhari, ulikamilika kujengwa mwaka 1976 na kuwa jengo refu linalosimama pekee kuliko yote duniani wakati huo.
Mnara huu ulishikilia rekodi hiyo ya dunia kwa miaka 34 mfululizo kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Burj Khalifa (urefu mita 829.8 ama futi 2,722) huko Dubai ambao ndio mnara mrefu kuliko yote duniani kwa sasa na Mnara wa Canton huko Guanzhou, China (urefu mita 600 ama futi 2000) ambao ni wa pili kwa urefu,  mwaka 2010. Ila hadi leo mnara huu unabakia kuwa ndio mrefu kuliko yote katika ukanda wa Magharibi, ukiwa alama kuu ya Toronto na nembo ya nchi ya Canada, ukivutia watalii takriban milioni mbili kwa mwaka.
Jina lake la CN linatokana na lile la Canadia National, ambalo ni shirika la reli la Canada lililoujenga. Kufuatia uamuzi wa kubinafsisha mali za shirika hilo mwaka 1995, umiliki wake ukahamishiwa kampuni ya ardhi (Canada Lands Company.
Mwaka 1995 mnara wa CN ukatangazwa kuwa moja ya maajabu saba ya dunia na jumuiya ya wahandisi wa majengo ya Marekani, na pia ni mojawapo ya majengo yaliyo chini ya Shirikisho la Minara Mikubwa duniani, mnara wa CN ukishika nafasi ya pili.



No comments:

Post a Comment