Bw Kiswaga mwenye suti kati na viongozi wengine wakitazama chumba cha kuhifadhia maiti katika hospital teule ya Iringa chenye jokofu lenye uwezo wa kuhifadhi maiti 6 pekee huku chumba hicho kikiwa hakina huduma ya maji wala mhudumu
MKAZI
wa Kalenga wilaya ya Iringa mkoani hapa Bw Jackson Kiswaga ametoa
msaada wa vitanda viwili vyenye thamani ya Tsh milioni 3.6 kwa
Hospital teule ya wilaya ya Iringa Hospital ya Ipamba ili kunusuru
wanawake wajawazito kujifungulia chini.
Kiswaga
ambae pia ni mkuu wa M-Pesa na ukuzaji wa biashara alikabidhi
msaada huo jana mbele ya uongozi wa Hospital hiyo na viongozi wa
kata hiyo ya Kalenga .
Bw
Kiswaga alisema kuwa amelazimika kutoa msaada huo wa vitanda
katika Hospital hiyo kama njia ya kuhamasisha wakazi wengine wa
wilaya ya Iringa ambao wapo nje ya mkoa wa Iringa kujenga utamaduni
wa kuchangia shughuli za kimaendeleo katika wilaya hiyo ya Iringa
na mkoa kwa ujumla badala ya kuendelea kuiachia serikali na
wahisani kufanya kila jambo hata yale ambayo yapo chini ya uwezo
wa wananchi wenyewe.
"Kuna baadhi ya shughuli za kimaendeleo
hazipaswi kusubiri serikali wala kusubiri wafadhili kutoka nje ya
Tanzania ...tujikipanga wenyewe wananchi tunaweza kufadhili shughuli
hizo huku serikali na wahisani wakubwa tukiwasubiri kwa mambo
makubwa ambayo sisi wananchi hatuwezi kuyafanya "alisema Kiswaga
Kuwa
akiwa kama mkazi wa jimbo la Kalenga alipata kulazwa katika
Hospital hiyo na moja kati ya changamoto kubwa alizokutana nazo
hapo ni pamoja na suala la upungufu wa vitanda na changamoto nyingine
nyingi hivyo kulazimika kwa upande wake kwa kushirikiana na
marafiki zake waliopo jijini Dar es Salaam kuchangishana fedha za
kununua vitanda hivyo vya kisasa ili kusaidia kupunguza uhaba wa
vitanda .
Aidha alisema kuwa ataendelea kuangalia uwezekano
wa kuisaidia zaidi Hospital hiyo ambayo ni mkombozi mkubwa kwa
wakazi wa jimbo la Kalenga na wilaya ya Iringa kwa ujumla na
kuahidi kusaidia kuingiza maji katika chumba cha kuhifadhia maiti
katika Hospital hiyo ambayo ina chumba chenye uwezo wa kuhifadhi
maiti sita pekee ila hakuna maji ya kusaidia kuosha maiti .
Hata
hivyo alisema kuwa msaada huo umelenga kusaidia jamii ya wana
Kalenga na mkoa wake wa Iringa na hauna malengo ya kisiasa na
kuwa baadhi ya watu wamekuwa na dhana potofu kuwa mtu
anapojitolea kusaidia shughuli za kimaendeleo nyumbani kwake kuwa
anataka nafasi ya kisiasa na kuwa katika hili mbunge wa jimbo hilo
la kalenga Dr Wiliam Mgimwa anatambua msaada huo .
Kwa upande
diwani wa viti maalum Tarafa ya Kalenga Shakra Kiwanga akishukuru
kwa niaba ya wakazi wa Kalenga alisema kuwa msaada huo ni chachu
kwa wadau wengine kuendelea kufika katika Hospital hiyo na jimbo
la Kalenga kuendelea kusaidia shughuli mbali mbali za kimaendeleo
na kumpongeza Bw Kiswaga kuwa amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika
tafara ya kalenga .
" Sisi kama wana kalenga tunaendelea
kukuombea afya njema na Mungu azidi kukuongezea pale unapopunguza
kwani huu ni msaada wa kwanza kutoa kwetu ulipata kutusaidia ujenzi wa
vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari ya Lipuli ....na
maeneno mengine mengi "alisema Bi kiwanga |
Ubarikiwe Sana, kutoa ni moyo imenigusa hiyo!
ReplyDelete