Monday, September 16, 2013

KINANA AWASHUKIA WATENDAJI WAZEMBE

  • ATAKA VIONGOZI WA CHAMA KUFANYA KAZI KWA KUJITOLEA
  • AWAAGIZA VIONGOZI WA CHAMA KUWA KARIBU NA MABALOZI WA NYUMBA KUMI
  • APONGEZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI
  • ASEMA KATIBA HAITABADILISHA MAISHA KAMA KUFUMBA NA KUFUMBUA MACHO. 
  • AWAAMBIA WATENDAJI WA SERIKALI HAWANA BUDI KUTEMBELEA WANANCHI BADALA YA KUJIFUNGIA OFISINI
  • ASIKITISHWA NA UZEMBE WA KUTOWAPA TAARIFA WANANCHI KWA WAKATI
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pole John Shilindi mtoto wa Balozi wa Shina namba 1 kata ya Dakama wilaya ya Maswa aliyefariki hivi karibuni.
 Kikundi cha Ngoma kikionyesha uwezo wake wa kucheza ngoma ya Pudini ambao ni wasukuma wachunga Ng'ombe wakati wa mapokezi ya Katibu mkuu wa CCM wilayani Meatu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili wilaya ya Meatu tayari kwa ziara ya siku moja wilayani hapo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupasua mbao baada ya kuzindua mradi wa ufundi selemala katika kata ya Bomani, wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana moja ya shina la CCM kati ya mashina mengi aliyofungua wilayani Meatu.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua Daraja la la mto Mwahnuzi ambalo ni moja ya sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais.
 Katibu Mkuu wa CCM akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiangalia nyumba zinazojengwa kwa ajili ya watumishi wa Halmshauri,wilayani Meatu.
 Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akihamasisha watu waliofurika kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Meatu mkoa wa Simiyu
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Meatu katika viwanja vya kituo cha mabasi cha Mwahnuzi mkoani Simiyu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo amesimikwa kuwa Chifu wa wasukuma wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu na kutambulika kama Chifu Kilabanya.
 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Mbunge wa Maswa Ndugu John Shibuda, Shibuda aliieleza hadhira kuwa Kinana ni rafiki yake mkubwa  na wasiku nyingi wakati Nape alielezewa kama mtoto wake kwani yeye na marehemu Nnauye walikuwa marafiki wa kushibana.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwahutbia wakati wa Mwanhuzi wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambapo Katibu Mkuu alipata nafasi ya kugusia suala la Katiba,matatizo ya maji na umeme ambayo vyote ameyapatia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment