Monday, August 12, 2013

WAZIRI MAGHEMBE AZINDUA BODI MPYA YA MAMLAKA YA MAJI MJINI MOSHI

Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akizungumza na wajumbe wapya wa bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)wakati wa hfla fui ya kuizindua bodi hiyo iliyofanyika katika ukumbu wa bodi wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) Cyprian Luhemeja akisoma taarifa mbele ya waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya mamlaka hiyo.
Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) Hajira Mbande ambaye pia ni meneja wa Azania Bank tawi la Moshi.
Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) cyprian Luhemeja ambaye pia ni mkurugenzi wa MUWSA.
Baadhi ya wageni pamoja na wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)wakifuatilia hotuba ya waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe wakati wa uzinduuzi wa bodi mpya wa mamlaka hiyo.
Wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi (MUWSA)katika picha ya pamoja na waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe.


Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi

WAZIRI wa maji Prof Jumanne Maghembe, amesema mara baada ya notisi ya miezi sita kumalizika,serikali italazimika kuzikatia maji baadhi ya taasisi zake likiwamo jeshi la polisi na magereza kutokana na kuwa na malimbikizo ya deni la Ankara za maji la zaidi ya Sh Bil 5.3 nchini kote.

Amesema taasisi hizo zilipewa notisi ya kuhakikikisha zinalipa malimbikizo yao kwa kipindi cha mwezi April hadi Septemba mwaka huu, lengo likiwa ni kuhakikisha mamlaka za maji zinazodai fedha hizo zinaweza kuendesha shughuli zake bila vikwazo vyoyote.

Prof Maghembe amesema hayo wakati akizindua bodi mpya ya wakurugenzi ya mamlaka ya majisafi na taka mjini Moshi(MUWSA), yenye wajumbe 10,ingawa pia alisisitiza umuhimu wa mamlaka za maji kutotanguliza suala la kuwakatia wateja huduma hiyo bali kuwaelimisha na kabla ya uamuzi wa kusitisha huduma.

Wajumbe wa bodi hiyo ni mwenyekiti, Shally Raymond,makamu mwenyekiti Prof Faustine Bee,katibu Cyprian Luhemeja, wengine ni Japhary Michael,Elizabeth Minde,Boniface Mariki,Alfred Shayo,Hajira Mmande,Abdala mkufunzi,Mtoi Kanyawana na Bernadette Kinabo.

“Hizi taasisi za serikali tunafahamu kwamba zinamadeni makubwa, ipo inayodaiwa hadi Mil 400, tayari tuliwapa notisi April hadi Septemba mwaka huu…tumewaeleza msipolipa tutakata huduma, maji ni gharama lazima yalipiwe ili mamlaka ziboreshe miundombinu yake” alisema Maghembe.

Mapema katika taarifa yake,mkurugenzi wa MUWSA ambaye pia ni katibu wa bodi,mhandisi Cyprian Luhemeja alisema mamlaka imejipa siku 180 za mabadiliko ambapo alimuhakikishia waziri kwamba hadi kufikia Disemba mwaka huu mamlaka itakuwa imepunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 39 hadi tisa.

Aidha mkurugenzi huyo alisema katika mpango wa matokeo makubwa sasa ‘Big result now’ pia wamekusudia kuongeza idadi ya wateja kutoka 21,000 hadi kufikia 35,000 ifikapo Disemba mwaka huu lengo likiwa ni kufikia wateja 50,000 ifikapo Juni mwaka 2014.

Naye makamu mwenyekiti wa bodi hiyo,Prof Faustine Bee, alisema bodi itahakikisha siku 180 zinatoa matokeo yaliyokusudiwa na kutaka wafanyakazi kutoa ushirikiano kwani miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele ni maslahi yao.

No comments:

Post a Comment