Thursday, February 14, 2013

UPDATES ZA SAKATA LA TFF PART I: WADAU WA SOKA WAMJIA JUU NAIBU WAZIRI AMOS MAKALLA


Wadau wa soka ambao wengi wao ni wachezaji wa zamani wamemtaka Naibu Waziri wa Habari Amosi Makalla kujiuzulu kwa madai ya kuingilia mchakato wa uchaguzi pale alipolitaka Baraza la Taifa la Michezo (BMT) na Rais wa TFF Leodegar Tenga kuingilia kati mchakato wa rufaa na kumrejesha Malinzi kwenye kinyang'anyiro huku akidai kuwa kamati hiyo ya rufaa imenunua dharau kwa gharama ndogo.

"Tumeshtushwa sana na tamko la Amos Makalla kwamba lazima Malinzi arejeshwe, kwa kanuni zipi ama chombo gani, mbona yaonyesha mgombea alikuwa na watu wake wengine mfukoni.


"Kanuni zilizotumika kumuengua Malinzi kwani ni mpya? au zimeshatumika tena kuwahukumu wengine kama wakina Amin Bakharesa kwa kupungukiwa sifa mbona hakutetea na hao wanaojiita wadau? Ama huyu tu kwa kuwa inalalamikiwa na wapambe wake amepata hasara, ipi wakati kampeni hazijaanza? walihoji.


"Yawezekana alipitishwa kimakosa kwenye kinyang'anyiro cha mwaka 2008 hiyo isiwe sababu ya kutohukumiwa sasa: "Mwanaume anapofumaniwa hawezi kujitetea kwa kusema mbona juzi nilikuwa naye na leo iwe kosa kukutwa naye? kosa ni pale inapothibitika na kutokea anayelalamika kuthibitisha kile kinachomtuhumu mtu.


"Sisi tunailaumu TFF tangu kelele hizi zinatokea za upotoshaji hawajasimama kufafanua maamuzi na vifungu vya kisheria vilivyowaengua watu, baya zaidi kamati ya uchaguzi nayo imesimamisha kampeni,TFF nayo imekaa kimya ama nao wana ajenda gani iliyojificha?


"Sepp Blatter wa FIFA mbona aligombea peke yake mara ya mwisho wakati mpinzani wake alipokatwa kwa tuhuma za rushwa, nalo lililiwa sahihi? kosa ni hapa kwetu Tanzania, tusirudishe enzi za FATA za migogoro, tumeona kazi ya Tenga nzuri kiasi kikubwa, sasa tunataka kuona mpira haya yanayoanza Simba, Azam na Taifa Stars zinaweza zikaathirika kwa kufungiwa Tanzania kwa watu wasio na mamlaka katika chombo huru.


Baadhi ya wachezaji wa zamani waliozungumza na waandishi kupinga hatua ya wadau wa soka kutaka Malinzi arejeshwe ni Fikiri Magoso, Abeid Mziba, David Mwakalebela, Makumbi Juma, Thomas Kipese , Mwanamtwa Kihwelo na Mohamed Hussei (Daima) wakati wadau ni Photonauts Mangwela diwani wa zamani wa Temeke, Bakili Makele, Abdulrahaman Kipenga na Saleh Ndonga

No comments:

Post a Comment