Thursday, February 14, 2013

mkutano wa tatu wa Wadau wa nssf ndani ya jiji la arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akisisitiza jambo mbele ya  Wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akifafanua jambo mbele ya wadau waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza jana Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.
Mbunge wa jimbo la Perahamio-Songea,Mh Jenista Mhagama akiomba kupewa ufafanuzi kuhusiana  na Sera na Sheria za fedha ziko salama kiasi gani katika mifuko ya hifadhi ya jamii,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Irene Isaka,akifafanua kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo mifuko ya hifadhi ya jamii,ikiwemo sambamba na namna gani inavyoweza kukuza uchumi na kuleta maendeleo makubwa ndani ya jamii.
Mchambuzi Mkuu wa masuala ya Kifedha kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT),Bi.Liku Katekamba akitoa ufafanuzi kuhusiana na usalama wa fedha ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii,na pia amewataka Wanachama kuwa na imani ya mifuko yao ya hifadhi ya jamii.


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha mahusiano NSSF,Eunice Chiume  wakati  wa mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab akifatilia kwa makini mada mbali mbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa mkutanoni hapo.

Pichani ni sehemu ya Wadau mbalimbali  zaidi ya 1000 waliohudhuria Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.
Waheshimiwa wakibadilishana mawazo.
Wadau mbali mbali wa mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),wakiwa wamesimama kwa dakika moja ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka aliekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Marehemu Sijaru Juma Kaboyonga.



 Mdau akipata taswirazzz za mkutano huo.











 Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa NSSF,Yacoub Kidula akiwasilisha mada yake.



 Wakurugenzi,Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Dkt. Ramadhan Dau na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF,Willim Erio.
Wadada wa NSSF,Kulia ni Dada Alice Simba na Agnes.
 Mkutano wa Wadau wa NSSF ukiendelea ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
 wakati mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ukiendelea ndanu ya ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,pia kulikuwa na huduma za matibabu na vipimo kwa wadau hao.
 Maofisa wa Usajili kwa Wadau wa NSSF,Bi. Violet Segema (kushoto) na Abdulrahman Suleiman wakiwajibika.
 Mdau Alison Kwilike (shoto) na Dada Grace Magigita wakipiga mzigo.
 Wadau wakichangia damu.

No comments:

Post a Comment