UTANGULIZI
Kutokana na mgomo wa
madaktari uliotokea kati ya tarehe 23 na 29 mwezi juni 2012.Wizara iliwasilisha
malalamiko kwenye Baraza la madaktari Tanganyika ili lifanye uchunguzi kuhusu
madaktari hao .Idadi ya madaktari wote waliogoma walikuwa 394, kati yao madaktari 376
walikuwa ni madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo (Interns) kutoka hospitali
za Muhimbili, K.C.M.C. Bugando, Mbeya Rufaa, St.Francis - Ifakara, Dodoma,
Temeke, Mwananyamala, Amana, Haydom na Sekou Toure. Aidha, Madaktari waajiriwa(Registrar)
18 walishiriki katika mgomo huo
kutoka hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Baraza
lilipitia malalamiko yote na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari
aliyethibitishwa kushiriki katika mgomo huo.
Adhabu hizo zilikuwa katika makundi yafuatayo; onyo, onyo kali na kusimamishwa
udaktari kwa muda wa kati ya mwezi mmoja na miezi sita.Vile vile kuna Madaktari
ambao hawakuwa na hatia ya kushiriki katika mgomo na hivyo walifutiwa mashtaka.
MCHANGANUO WA ADHABU
- Waliofutiwa
mashitaka madaktari 49
- Waliopewa
onyo madaktari 223
- Waliopewa
onyo kali madaktari 66
- Kusimamishwa
kwa muda madaktari 30
- Mashitaka
yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria
madaktari 4
- Mashitaka
yasiyosikilizwa kutokana na
wahusika kutofika walipoitwa na Baraza
madaktari 22
Wizara
inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma kwa
Madaktari wote waajiriwa ambao walipatikana na hatia mbele ya Baraza la
Madaktari. Wizara pia imeridhia kuwapa
Madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na
mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa. Hata hivyo fursa hii haitawahusu Madaktari
wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari, hadi hapo
watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
HITIMISHO
Kwa
taarifa hii madaktari wote waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo
kali wanatakiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
barua kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa
usajili na kuruhusiwa kuendelea na
mafunzo kwa vitendo. Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ili kupewa barua zao kulingana na Adhabu
walizopewa. Barua hizi zitatolewa kuanzia tarehe 2 Januari, 2013.Madaktari wote
walio katika mafunzo kwa vitendo wanatakiwa kuanza kazi katika vituo vyao vya awali
ifikapo tarehe 14 Januari, 2013.Hakuna muda utakaoongezwa kwa kipindi
kilichobakia cha mafunzo kwa vitendo. Kwa wale wote waliopewa adhabu
wataanza kutumikia adhabu hizo kuanzia tarehe ya adhabu hiyo ilivyotolewa.
Nsachris
Mwamwaja
Msemaji
WIZARA YA AFYA NA
USTAWI WA JAMII
27/12/2012
Maamuzi sahihi ingawa yamecheleweshwa na madaktari wenyewe kusuasua kuchukua hatua stahiki. Sasa turudi kazini kuwahudumia watanzania, tufuate taratibu muafaka kudai haki zetu. Tanzania itajengwa na mtanzania...
ReplyDeleteimetulia
ReplyDeleteSerikali inawaogopa tu..wangewapiga ata mwaka kwa kushindwa kugoma ipasavyo na kusalitiana..shame upon them
ReplyDeleteNiliwahi waambia watanzania wengi kuhusu njia iliyotumika ya madaktari kudai haki yao haikuwa sahihi kabisa kulingana na asili ya kazi zao!...ile haikuwa siasa kugoma kwa daktari ni aibu mno na hushusha status ya kazi yao, tazama watu walivyokuwa wakiteseka na pengune wengine walikufa kabisa kama kweli wao ni madaktari iko wapi huruma yao???Nilikerwa sana kipindi kile roho ilikuwa inaniuma sana jinsi mbavyo watu walikuwa wakiumia!!!nimefurahishwa sana na maamuzi hayo tena mimi binafsi naona dhabu hizo hazitoshi,...
ReplyDelete