Thursday, December 1, 2011

Airtel yafikisha zaidi ya wateja milion 50 Afrika

Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Limited
Manoj Kohli 

Bharti Airtel Limited (“Airtel”), kampuni ya simu za mkononi Airtel yenye kuendesha biashara zake katika nchi 19 barani Afrika na Asia leo inasherehekea mafanikio makubwa iliyoyapata Afrika kwa kufikisha zaidi ya wateja million 50 ikiwa tu ni mienzi 17 mara baada ya kuinunua Zain Afrika iliyokuwa inaendesha huduma zake katika nchi 16 Africa. Airtel imeweza kuongeza zaidi ya wateja wapya milion 14 ndani kipidi hiki.

“Mafanikio haya yameonyesha nia na dhamira yetu katika kuendeleza mawasiliano Afrika. Alisema Mr. Manoj Kohli ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Limited. “ Tunawashukuru wateja kwa kuwa na imani na Airtel na tunawaahidi kuendelea kuwapa huduma bora , pia tunapenda kuishukuru serikali na mamlaka za mawasiliano kwa ushirikiano wao unaotuwezesha kuendelea kutoa huduma za kisasa kwa gharama nafuu kila siku”.

“Tumewekaza kwa kiasi cha kutosha katika sehemu zote tunazofanya biashara kwa lengo la kutoa huduma nzuri ya kimataifa Afrika nzima” alisema Bw Manoj.

Airtel itaendelea kutoa huduma za kisasa za simu za maongezi na data ili kuendelea kuleta mafanikio mazuri zaidi kwa wateja wake na kuongeza thamani katika shughuli zao na maisha yao ya kila siku”.

Ni kwa sababu hiyo Airtel imeweza kupata tuzo mara mbili ambazo ni global mobile awards for innovation mwaka uliopita wakati wa tuzo za GSMA kule Barcelona. Pia Airtel imeweza kupata sifa ya kuwa moja ya kampuni inyotoa huduma bora ya Kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja kwa kujiwekea utaratibu na mahusiano bora na wateja wake.

Kutokana na uhusiano wa kimkakati kati yetu na mashirika ya bluu Chip, kampuni inauhakikisha kwamba itaendelea kukidhi mahitaji ya wateja wake kwa kuwa Mfumo wa Biashara Airtel unalenga kubuni na kuanzisha bora ili kuweza kukidhi soko la kimataifa. Shirika hilo huweka mikakati ya kibiashara na makampuni kama vile IBM, Ericsson, Nokia Siemens, Huawei, Spanco, Tech Mahindra na Samsung. 

Bado ushirikiano utaendelea ili kutoa na kuanzisha teknolojia za kisasa na kutoa huduma zenye kukidhi ushindani uliopo kwa kuzingatia maeneo ya msingi ndani ya biashara.

Airtel Afrika imewekeza zaidi ya dola bilion moja katika kuendeleza miundombinu kwenye mtandao wake na mwaka huu wa fedha inazindua huduma za technologia bora kama zile zinazopatikana Europe na USA kwa sasa. 

Airtel imeshakabidhiwa leseni 12 za 3G katika nchi zinazotoa huduma zake na hivi karibuni imezindua huduma ya mtando wa 3G Congo mapema mwaka huu. Vilevile Airtel inaongeza matawi yake zaidi baada ya kupata leseni ya kuanzisha huduma za simu (GSM network ) nchini Rwanda mbali na kujenga miundombinu muhimu, Airtel imesaini mikataba na makampuni makubwa kama zile Nokia, Samsung and Blackberry ili kuweza kutoa vifaa vitakavyowawezesha wateja wake kupata huduma kwa uhakika.

Mbali na hapo Airtel imeanzisha mipango mathubuti ambayo inavutia jamii ya Afrika na kuwapa hamasa, kupitia miradi mbalimbali kama vile Airtel Rising Stars. Airtel Rising Stars ni mpango kabambe Afrika wenye lengo la kuinua vipaji inayolenga katika kugundua na kuendeleza vipaji vya vijana katika umri mdogo na kuwajenga kuwa bora katika ngazi ya taifa.

Afrika ina watu wapatao billion 1 na pia ni bara lenye wakazi wengi wenye umri mdogo duniani. Watu wenye umri chini ya miaka 25 ni Asilimia 60 ya jumla ya idadi ya watu Afrika ukilinganisha na nchi zilizoendea ambazo zina asilimia 30%.ukiacha China na India, Africa ni bara linalokuwa kwa kasi kiuchumi Dunia. Takwimu hizi zilizotolewa na IMF’s World Economic Outlook 2011

No comments:

Post a Comment