Wednesday, November 30, 2011

JERRY MURO MARA BAADA YA KUFUTWA KWA KESI YAKE

Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Jerry Muro na mke wake wakitoka mahakamani.
Mmoja kati ya watuhumiwa waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya shilingi milioni kumi, Edmund Kapama akitoka katika chumba cha Mahakama huku akina na furaha kwa kuwa huru.
Nipo huru sasa.
Pascal Kamara wakili wa Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya kisutu.
Pokea Mvinyo Baba.

Waandishi wa habari wakiwa Mahakamani hapo 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewaachia huru kwa mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jarry Muro na wenzake wawili.

Hakimu Frank Moshi, alisema anawaachia washitakiwa hao kwasababu upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi shaka.

Muro, Edmond Kapama pamoja na deogratius Mgasa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba na kutaka kupokea rushwa ya Sh milioni 10 toka kwa aliyekuwa Muhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage.

Mashitaka yao yalikuwa ni ya kula njama, kuomba rushwa na kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU shitaka linalowakabili Mgasa na kapama.

Muro baada ya kutoka mahakamani alitangaza kwa wanahabari kuwasamehe wabaya wake wote ambao ni viongozi wa serikali baadhi na baadhi ya maafisa wa polisi na kuwataka waandishi wa habari kushikamana kuendelea kuibua uozo unaoendelea bila woga.

Katika hukumu, hakimu Moshi alisema baada ya kuangalia ushahidi mahakama ilikuwa na maswali ya kujiuliza kama upande wa jamuhuri uliweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa ambapo shitaka la kula njama kwa nia ya kuomba rushwa ambalo linawahusu washitakiwa wote, ushahidi ulikuwa wa Wage.

Shahidi huyo wa tatu wa jamuhuri lisema alikutana na Muro kwenye mgahawa wa Califonia ambapo mawasiliano kati yao yaliendelea kwa njia ya simu ya mkononi. 

Ushahidi huo ulikuwa hafifu kwasababu upande wa mashitaka haukuweza kuwasilisha karatasi ya mawasiliano kati yao kutoka kwenye kampuni ya mtandao wa simu (printout).

Vile vile alisema picha za CCTV iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa ni kivuli kisichoonyesha sura za watu badala yake wangeleta CD kuonyesha kwenye video ili watu waweze kutambulika kwa urahisi. 

Mawasiliano ni jambo la msingi kwasababu ili kula njama ni lazima mawasiliano yafanyike hivyo kuna mapungufu makubwa katika shitaka hilo.

Dereva aliyemwendesha wa Wage alidaiwa kuwa na Wage pale mgahawa wa Califonia walipokutana na Muro, alitakiwa kuletwa athibitishe kama Wage na Muro walikutana upande wa mashitaka hawakumwita shahidi huyo.

Katika shitaka la kuomba rushwa lilowakabili wote katika ushahidi wake Wage, alieleza Muro na wenzake walimtaka awapatie Sh milioni 10 watamsaidia kwenye tuhuma zinazomkabili lakini hakuwa nazo akawapa sh milioni moja mbali na ushahidi huo hakuna ushahidi mwingine wa serikali unaoonyesha kuwa walipokea fedha hiyo.

“Mahakama ilitegemea kuwe na ushahidi wa mawasiliano kama haupo wa kuona lakini hayo yote hayakufanyika,” alisema hakimu Moshi.

Muro alikamatwa ndani ya gari, mahakama haielewi ni kwanini kulikuwa na haraka hiyo kwanini asingeachwa wakakutana na Wage. Kwa upande wa hotel ya Sea Cliff ni sehemu ya watu yoyote anaweza kwenda.

Washitakiwa Mgasa na Kapama hakimu Moshi alisema hawakukamatwa eneo la tukio walikamatwa na kuunganishwa na halikufanyika gwaride la kuwatambua na cheti kuletwa mahakamani.

Shitaka la linalowakabili Mgasa na Kapama la kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU mahakama ilisema halikuthibitishwa lina mashaka. Alisema washitakiwa walijitambulisha kwa moja anaitwa Dr na mwingine Musa.

Upande wa mashitaka ulitakiwa kufatilia mtaani kama majina hayo washitakiwa walikuwa wakiyatumia lakini hilo halikufanyika.

“Wage kama msomi ngazi ya uhasibu aliwezaje kukubali mtu ajitambulishe kwa mdomo kama afisa wa TAKUKURU bila kuonyeshwa vitambulisho na akakubali mahakama inapata mashaka”. 

Aliongeza hakimu huyo hakuna vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha bila kuacha shaka hivyo wanaachiwa huru kwa mashitaka yote.

Alisema Moshi risiti, pingu na miwani havikuwa na mgogoro katika kesi na kwavile vilipatikana kwa risiti basi arudishiwe muhusika na upande unataka kukata rufaa wana ruhusiwa. Wakili kiongozi wa kesi hiyo Boniface Stanslaus alisema taafifa atampelekea Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ataamua kama watakata rufaa.

Washitakiwa walifikishwa mahakamani Februari 5 mwaka jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu mkazi, Gabriel Mirumbe.

12 comments:

  1. Tunashukuru haki imetendeka, Nimefurahi sana kukuona uko huru kaka, nakufunika kwa damu ya yesu wabaya wako wote wataaibika. Hongera sana kaishi kwa amani na mkeo bro.

    ReplyDelete
  2. haki ya mtu haipotei bali hucheleweshwa.
    hongera sana kwa ushindi na hongera kwa kua na mke mwema hapo ndo pale tunasema "katika shida na raha"huyo ni mke mwema.
    kamwe usikate tamaa na hicho kilikua kikwazo cha kukufanya uwe strong zaidi.

    be blessed always.

    linda.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana my Brother sio siri nimefurahi kupita maelezo acha sasa waangaike watafute mwingine wa kumbambikia kesi!Tanzania yetu watu chuki hawataki maendeleo ya mtu walijua utalositi sasa ndio kazi imeanza!kaza buti baba Mungu yupo pamoja nawe. Big up.

    ReplyDelete
  4. Wow! Polisi wala rushwa walitaka kumwingiza ktk hatia bandia. Mungu ni mkubwa.

    ReplyDelete
  5. Big up Jerry, Hakika penye haki daima itacheleweshwa lakini utaipata.Big up kwa ushindi huo

    ReplyDelete
  6. pole kwa misuko suko Jerry, anza upya na kazi zako, upate mafanikio hata uwashangaze hao wenye tabia mbaya ya kuharibu maisha ya watu na future plans zako

    ALL THE BEST BRO & never say never........xoxo

    ReplyDelete
  7. Mdau BuckinghamshireNovember 30, 2011 at 5:17 PM

    Safi sana! Inaonekana Tanzania sasa hivi haki inatendeka (1) Kikwete kakubali maoni ya CHADEMA kuhusu suala la Katiba, (2) Mahakama imemwachia Jerry Muro!!

    This is very encouraging uncle Michuzi. Sasa kama mambo yakiendelea hivi wallahi na mimi narudi nyumbani nije nifanyie shughuli zangu za computing nyumbani.

    Mdau wa Buckinghamshire.

    ReplyDelete
  8. Mungu amekujalia ndugu yangu leo hii kuwa huru, kuna usemi usemao "ukweli ukiwepo uongo hujitenga" na Wanaokwenda jela sio wote wahalifu na hao waliokuzulia kesi washindwe na walegee. HILI NI FUNDISHO KWA KILA ANAYEMUONEA MNYONGE

    ReplyDelete
  9. hongera Jeri muro,mahakama
    ujumbe kwa Viongozi na walioweka
    "NI RAHISI KUMWELIMISHA ASIYEJUA AKAELEWA KULIKO KUMFANYA ANAYEJUA KUTOJUA"
    SIKU MOJA VIONGOZI WATAKUWA BENDERA NA SISI TUTAKUWA UPEPO;KAMA HAWAAMINI WASUBIRI KUONA KWA VITENDO:
    HUKUMU HII NI FUNDISHO KWA POLISI KUWA WASITUMWE ILA WASIMAMIE HAKI BILA KUSHURUTISHWA NA YEYOTE KWA SHERIA LAZIMA IBALANSI:HII NI AIBU KUBWA KWA MBELE YA WALIPAKODI:
    JE WANAWEZA KUTOA TADHMINI YA GHALAMA YA KESI YA KIPUUZI KAMA HII:
    HARAFU MISHARA YAO HAITOSHEREZI;WANAISHI KWENYE MABATI
    :
    LAKINI MTAAMKA SIKU MOJA NA KUJUTA KWA NINI MNATUMIKIA WASIOTUMAINIKA

    ReplyDelete
  10. Bwana Muro Hii ni Tanzania zaidi ya uijuavyo. Sijui Kova anajisikiaje. Nilitegemea Mwema akusaidie baada ya kumsaidia kufichua uozo. Du kumbe lao ni moja tu. Sasa hivi watakubambikiza kile kibiashara chao vijidawa kaa chonjo.....Ningelikuwa Rais wa nchi ningeliingia kati kwenye kesi hii. Pole kamanda!

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Jerry n wenzako lakini kama ambavyo umeahidi go ahead nchi yetu ni nzuri ila inaharibiwa na wachache!!

    ReplyDelete