Mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Shinda mtaji’, Godfrey Kitende akionesha hundi ya Sh milioni aliyoshinda baada ya kukabidhiwa jana na Kampuni ya Selcom inayoshirikiana Mastercard kutoa zawadi kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR.
Mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Shinda mtaji’, Godfrey Kitende akipokea hundi ya Sh milioni kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Selcom, Juma Mgori. Kampuni hiyo inashirikiana Mastercard kutoa zawadi kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR
Kampuni ya Selcom kwa kushirikiana na Mastercard imetoa zawadi ya Sh milioni tatu kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR katika kupokea malipo mbalimbali kwenye maeneo yao ya biashara.
Zawadi hizo zimetolewa jana katika promosheni ya “Shinda Mtaji” iliyoanza rasmi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuwarahisishia wafanyabiashara hao kutumia huduma ya Masterpass QR kufanya miamala mbalimbali.
Akizungumza promosheni hiyo, Meneja Masoko wa Selcom, Juma Mgori alisema promosheni hii inamuwezesha mfanyabiashara kujishindia Sh milioni moja kila wiki kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Novemba mwaka huu hadi Januari mwaka 2019.
Aidha, aliwataja wateja walioshinda milioni moja kila mmoja kuwa ni Boaz Wales, Hamisi Kilenga wote wa mkoani Dar es Salaam na mfanyabiashara mmoja kutoka Arusha.
Alisema kila mfanyabiashara atakayejiunga na Masterpass QR na kuanza kupokea miamala kutoka kwa wateja, ataingia moja kwa moja kwenye droo ya promosheni kwa wiki hiyo na kupata nafasi ya kujishindia hivyo kumuwezesha kujiongezea mtaji wa biashara yake.
“Masterpass QR ni huduma inayomuwezesha mteja kufanya malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka kwenye akaunti ya simu au akaunti ya benki kwa kuingiza Pay Number ya mfanyabiashara au ku-skani kodi ya QR iliyopo kwenye eneo la mfanyabiashara kwa kutumia Smartphone.
“Kupitia huduma ya Masterpass QR, mteja ataweza kufanya malipo kupitia mitandao ya simu kutoka Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, Halopesa, Ezypesa na Selcom Card.
Aidha, alisema kwa upande wa huduma ya mobile banking mteja ataweza kufanya malipo kutoka Access Bank, I&M Bank, NBC Bank, Akiba Commercial Bank, Amana Bank, BancABC, Canara Bank, Exim Bank, TPB Bank, NMB Bank, FINCA Microfinance Bank na Standard Chartered Bank.
“Wateja wa benki hizo pia wataweza kupakua Masterpass Tanzania App kupitia Smartphone na kujisajili ili kufanya malipo kwa Masterpass QR moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao za benki,” alisema.
Aliongeza kuwa ili mfanyabiashara aweze kusajiliwa na huduma ya Masterpass QR atatakiwa kujaza fomu ya kujiunga ambayo inapatikana kwenye ofisi za Selcom, atawasilisha leseni ya biashara, hati ya TIN na kitambulisho chake na itachukua siku 2 hadi 3 kuunganishwa na huduma ya Masterpass QR,” alisema.
Mmoja wa washindi hao Boazi Walesi alisema huduma ya Masterpass QR imemwezesha kuwaondoa adha ya kubeba fedha taslimu au kuwa na kadi ya benki muda wowote wanapohitaji kufanya malipo.
“Pia imeondoa usumbufu na gharama pamoja na kuleta usalama kwa wafanyabiashara ambao walikuwa wakikaa na fedha nyingi sehemu zao za biashara,” alisema.
Naye Hamisi Kitenga alisema mfanyabiashara anapojiunga kutumia huduma hiyo fedha za mauzo ya siku zitatumwa kwenye akaunti yake ya benki au simu siku hiyo hiyo baada ya siku ya kazi kuisha.
No comments:
Post a Comment