Monday, December 3, 2018

NAIBU WAZIRI MIFUGO NA UVUVI AWAPONGEZA MIKOCHENI ENGLISH MEDIUM SCHOOL KWA NAMNA INAVYOWANDAA WANAFUNZI KIELIMU

Na Said Mwishehe.

UONGOZI na walimu wa Shule ya Mikochen English Medium ya jijini Dar es Salaam wamepongezwa kwa kuendelea kufavya vizuri kielimu ambapo imekuwa ya pili kiwilaya, tano kimkoa na 54 kitaifa katika kundi la shule zenye watoto chini ya 40 katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba.

Pia wamepongezwa kwa kuwandaa wanafunzi katika misingi ya dini na malezi bora wakiwamo wa hitimu wa elimu ya msingi ambao wamefanya mahafali ya grade seven ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Uvuvi Abdalah Ulega.

Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa mahafali ya shule hiyo ambapo pia viongozi na walimu wamepongezwa kwa namna wqnavyowaandaa wanafunzi katika kuhakikisha wanazingatia masomo.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Ulega, Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi kutoka Wizara ya Kilimo na Mifugo Zacharia Kera amesema anaipongeza shule hiyo kwani imepiga hatua kimaendeleo na hasa katika kuwaandaa wanafunzo wake kitaaluma.

Wakati wa mahafali hayo wazazi na walezi wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha wanashuhudia mahafali hayo huku mgeni rasmi akitumia nafasi hiyo kutoa pongezi pia kwa walimu waliofanikisha kuwajenga kielimu wanafunzi ambao wamehitimu shuleni hapo.

Kera amesema amefurahishwa na namna ambavyo wanafunzi wa shule hiyo wakiwamo wahitimu wa shule ya hiyo ambavyo wameandaliwa vema na kwamba wamejengwa kwenye misingi imara ya kielimu.

Amewataka wahitimu hao kutambua elimu ndio msingi wa maisha na hivyo wahakikishe wanasoma kwa bidiii kwani mchango wao unahitajika katika kulitumikia taifa kwa siku zijazo huku akioneshwa kufurahishwa na mafunzo ya lugha mbalimbali za kimataifa ambayo yanatolewa shuleni hapo.Amefafanua ili kuendana na dunia ya ushindani ambayo inahitaji mawasiliano ni vema mtu akafahamu alau lugha mbili za kimataifa ambazo zitamuwezesha kuwasiliana na mataifa mengine.

Pia Kera ameeleza kuwa mzazi au mlezi anatamani kuona mtoto anapata elimu bora,hivyo ameisifu shule hiyo kwa namna ambavyo inatambua kuwaandaa wanafunzi kwenye msingi wa masomo."Najua lengo la mzazi ni mtoto wake kupata elimu nzuri.Niwapongeze viongozi na walimu wa shule ya Mikochen English Medium kwa namna mnavyojitahidi kutoa elimu ambayo imeambatana na misingi ya malezi yaliyobora," amesema.

Pia amehimiza watoto kulelewa katika misingi ya dini na kwamba shule hiyo ni mfano bora huku akiwataka wanafunzi kutokata tamaa huku akiwahimiza walimu kuendelea kuwalea wanafunzi wa shuleni hapo kwa kuwajenga kimaadili.Ametumia nafasi hiyo kuhimiza wazazi kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu na kwamba wawe wanadai risiti kwa miamala ambayo wanaifanya.Kuhusu ombi la kompyuta ambalo limetolewa na uongozi wa shule hiyo, Kera amesema ombi hilo atalifikisha kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na anaamini atakuwa sehemu ya watakaosaidia kutafuta ufumbuzi wa ombi hilo.

Kwa upande wa uongozi wa shule hiyo umeeleza kufurahishwa na hatua mbalimbali za kimaendeleo huku wakizungumzia namna ambavyo wamefaminikiwa kwa wahitimu wao kufanya vema kwenye masomo kwa kupata alama za juu katika mitihani ya Taifa.Wakati huo huo walimu ambao wamewezesha wanafunzi kupata alama A kwenye masomo yao wamezawadiwa fedha ambapo kila alama ya A thamani yake ni Sh.25, 000.

Hivyo mwalimu wa somo la hesabu katika darasa la saba shuleni hapo ambaye amefanikisha wanafunzi wake kupata alama A 26 na hivyo uongozi wa shule mmempa fedha zaidi ya Sh.600,000 kutokana na jitihada zake za kuwafundisha wanafunzi hao ambao wamefanya vema kwenye mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi.
Mkuu wa shule ya msingi   Mikocheni English Medium, Zuwena Khamis Omar akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mahafali dalasa la saba yaliyo fanika mikocheni jijini Dar es Salaam. Shule hiyo imekuwa ya  pili kiwilaya, tano kimkoa na 54 kitaifa.
Sehemu ya wazazi na walezi wakiwa katika mahafali ya darasa la saba katika Shule ya Mikochen English Medium iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa katika mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika katika Shule ya Mikochen English Medium ya jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Zacharia Kera akizungumza na waandishi wa habari katika mahafali ya darasa la saba ya shule Mikocheni English Medium ambapo amewataka wahitimu kuwa na nidhamu, bidii na kutanguliza uzalendo katika yale watakayokuwa wakifanya ili kufikia malengo yao. (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG).
Sehemu ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya dalasa la saba katika shule ya Mikochen English Medium iliyopo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment