Saturday, November 3, 2018

Shirika la SBFIC kuwajengea uwezo watanzania kuhusu huduma za kifedha



Na George Binagi-GB Pazzo

Shirika la “Savings Banks Foundation for International Coorperation- SBFIC” lenye makao yake makuu nchini Ujerumani, limefungua rasmi ofisi yake nchini Tanzania lengo likiwa ni kufikisha karibu huduma zake  kwa watanzania.

Hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo ilifanyika Novemba Mosi 2018 katika eneo la Bwiru Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, yalipo makao makuu ya shirika hilo hapa nchini huku makao makuu ya Afrika Mashariki yakiwa Kigali nchini Rwanda.

Mkurugenzi wa shirika hilo hapa nchini, Stephen Noel Safe alisema limejikita kuwajengea uwezo wananchi pamoja na watoa huduma za kifedha kutekeleza miradi endelevu ili kutambua umuhimu na matumizi sahihi ya mikopo pamoja na kujiwekea akiba hususani kwa taasisi ndogondogo ikiwemo Vicoba.

Mgeni rasmi, Mtendaji Mkuu shirika la SBFIC, Dkt. Christoph Gogler kutoka nchini Ujerumani alisema huduma za shirika hilo zimewafikia wanufaika zaidi ya 2000 kwa njia mbalimbali ikiwemo mafunzo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuendeleza miradi yao kupitia huduma za kifedha ikiwemo mikopo na kujiwekea akiba.


Mkurugenzi wa shirika la SBFIC hapa nchini, Stephen Noel Safe akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mtendaji Mkuu shirika la SBFIC, Dkt. Christoph Gogler akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mtendaji Mkuu shirika la SBFIC, Dkt. Christoph Gogler akizungumza kwenye hafla hiyo.
Steven Revelian amnaye ni Mtendaji Mkuu mradi wa KARUDECA kutoka mkoani Kagera akiwasilisha salamu zake kwenye hafla hiyo.
Mudita Cheyo kutoka taasisi ya kifedha ya Self Entrepreneur akizungumza kwenye hafla hiyo namna taasisi yake inavyoshirikiana na shirika la SBFIC.
Viongozi wa shirika la SBFIC.
Mkurugenzi wa shirika la SBFIC hapa nchini, Stephen Noel Safe akieleza njia mbalimbali zinazotumika kufikisha elimu/ mafunzo kwa wananchi/ wanafunzi.
Mtendaji Mkuu shirika la SBFIC, Dkt. Christoph Gogler akiangalia machapicho yayotumika kufundishia.

Ofisini
Mgeni rasmi akisaini kitabu cha wageni.
Baadhi ya wafanyakazi shirika la “Savings Banks Foundation for International Coorperation- SBFIC”
Wanafunzi kutoka shule ya Msingi Karagwe mkoani Kagera ni miongoni mwa wanufaika wa mafunzo kutoka shirika la SBFIC
Kula keki kuashiria uzinduzi wa ofisi yetu.
Tazama video hapa nchi

No comments:

Post a Comment