Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo
cha Usalama Barabarani Taifa, anamuwakilisha kamanda wa kikosi cha
usalama wa barabarani Taifa akizindua rasmi shughuli hizo za upimaji wa afya kwa madereva wasafirishao mizigo masafa ya mbali iliyoandaliwa na North Star alliance kwa kushirikiana na Puma Energy Foundation , Impala Terminals na Trafigura Foundation.
Ndg. Henry Mgala Bantu mtaalam wa usafirishaji na uchukuzi na mbobezi wa
usalama barabarani na Mjumbe wa Balaza la taifa la usalama barabarani na
mwenyekiti wa elimu mafunzo na uenezi katika balaza hilo, akiwakumbusha madereva mambo mbalimbali muhimu yahusuyo Sheria za barabarani na somo muhimu la madereva kujitambua.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi Abben Swai Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania, akiendesha chemshabongo fupi kwa madereva wa magari ya mizigo yaendayo safari ndefu lengo ni kuwakumbusha tu kuendelea kuwa makini pindi wawapo safarini.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi Yoronimo Kwesibaga Saimon Mkuu wa kituo cha Polisi Bandari, akitoa salam zake wakati wa wiki ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya barabarani
Dkt. Sist Agustino Mosha Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Temeke akitoa elimu wa madereva wasafirio safari za mbali kuhusu umuhimu wa kutambua afya zao kipindi chote wawacho safarini, pia kuwakumbusha kutazama afya zao mara kwa mara kabla hawajaanza safari, mwisho aliwakumbusha madereva kuhusina na UKIMWI.
Mratibu wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama wa Barabarani(RSA) kanda ya Mashariki Bw. David Shao akielezea kwa ufupi umuhimu wa kuwa Balozi wa maswala ya Usalama barabarani na kuwaomba madereva wengi zaidi na watu wengine kujumuika kwa pamoja na kuwa mabalozi ili kusaidia kupunguza ajali.
Bw. Mohamed Sharif Mwenyekiti Chama cha Madereva Tanzania na Mkufunzi wa Masomo ya usalama barabarani, akisisitiza kuwa kongamano hilo ni muhimu sana kwa kuwa watu mbalimbali wakiwemo askari wa usalama barabarani, madaktari na watu wengine wameungana na madereva ili waje kuwapa elimu na kuwakumbusha mambo muhimu yahusuyo usalama wa barabarani na kujua afya zao maana ni mambo muhimu na yanayoendana kwa ukaribu.
Mwakilishi kutoka Impala Terminals akitoa salam zake wakati wa mkutano huo, amewashukuru North Star Alliance pamoja na wahusika wa Usalama kwa ajili ya kuhakisha madereva wanasafiri wanapata huduma ya afya kila wawapo safarini na ndio maana katika yard mbalimbali hata mikoani kuna ofisi za North Star alliance, aliomba ushirikiano huo uendelee zaidi.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi Abben Swai Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania(kulia) akisikiliza majibu ya chemsha bongo kutoka kwa mmoja wa madereva
Madereva pamoja na wageni wengine waalikwa wakiwa katika wiki ya kuelekea siku ya Usalama na Afya barabarani katika viwanja vya Impala Terminals
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP
Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo
cha Usalama Barabarani Taifa, akijiandaa kuendesha Scania ikiwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya siku hiyo.
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP
Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo
cha Usalama Barabarani Taifa, akiwa anaendesha Scania hilo.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi Abben Swai Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania (kushoto) akiwa ndani ya Scania kupata maelezo namna ya kuendesha Gari hilo kutoka kwa mtaalam wa magari hayo Bw. Patric.
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP
Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo
cha Usalama Barabarani Taifa akiwa anaungana na madereva wengine kupima afya zao.
Madereva wa Magari ya mizigo yaendayo safari za mbali pamoja na baadhi ya watumishi wa makampuni ya usafirishaji wakipima afya katika mahema ya North Star Alliance. (Picha zote na Fredy Njeje)
No comments:
Post a Comment