Thursday, October 11, 2018

WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA

Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye jengo la utawala la shule ya sekondari Kawawa wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa jeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kawawa iliyopo Mafinga Mkoani Iringa.
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja
Na hili ndio jengo la kisasa la utawala la shule ya sekondari ya kawawa lililofunguliwa na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi




NA FREDY MGUNDA,IRINGA.



WAZIRI wa ulinzi na jeshi lakujenga taifa Dr Hussein Mwinyi ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari yaKawawa kwa ujenzi wa jengo la kisasa la utawala ambalo litachangia katika ufanisi bora wa kazi kwa walimu na wafanyakazi wote wa shule hiyo.

Akizungumza wakati wa kuzindua jingo hilo la utawala waziri Mwinyi alisema kuwa jengo limejengwa kwa viwango ambavyo serikali ya awamu ya tano inataka na jingo hilo linaviwango vinavyotakiwa.“Kwa kweli nisiwe mchoyo wa fadhila jengo hili limejengwa kwa kuzingatia ujenzi unaotakiwa na lina ramani ambayo itadumu kwa miaka mingi na itakuwa auheni kwa wafanyakazi kufanya kazi zao kwenye jengo hili” alisema Mwinyi

Waziri Mwinyi aliwataka wafanyakzi wa shule hiyo kuhakikisha wanalitunza jengo hilo pamoja na miundo mbinu yake kwa ajili ya vizazi vingine. Awali akisoma risala kwa waziri Mwinyi mkuu wa shule hiyo Meja Erenest Sikaponda alisema kuwa jengo hilo la utawala limejengwa kwa shilingi 222,591,000 na kufanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 103,360,000 kwa kuwa hapo awali BOQ ilikuwa inaonyesha kuwa gharama za jengo ni shilingi 325,951,000.

Kupungua kwa gharama hizo ni kutokana na ubunifu,matumizi mazuri ya rasilimali,nidhamu katika matumizi ya fedha,nguvu kazi ya vijana ambao baadhi yao walikuwa mafundi na gari kubwa la kusombea mchanga,kifusi na mawe msaada huo ulitoka katika kikosi cha 841kj Mafinga” alisema Maj Sikaponda Maj Sikaponda aliwashukuru wadau mbalimbali ambao walitoa msaada wa hali na mali kusaidia ujenzi wa jengo hilo la kisasa la utawala ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa shule hiyo.

“Mheshimiwa waziri tunapenda kuwashukuru wadau wafuata TANROAD mkoa wa Iringa kwa msaada wa kifusi cha kujaza msingi kwa trip mia,kampuni ya kichina inayojenga barabara ya Mafinga Igawa kwa msaada wa tripu moja ya kokoto ya ujazo wa Mita 15 za mraba,Clement 
Sangale saruji mifuko 20, na Beruto Kaboda alitoa mbao 2×3 Arobain” alisema Maj Sikaponda

Aidha Maj Sikaponda alisema kuwa jengo hilo la kisasa la utawala linakabili na changamoto ya ukosefu wa samani kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo walimuomba waziri kuwasaidia kuzipata samani hizo.Tumalizie kwa kumshukuru mkuu wa JKT Tanzania pamoja na bodi ya shule kwa usimamizi mzuri wa mipango ya maendeleo ya shule hii.

Kwa upande wake mkuu wa JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu liwapongeza viongozi waliosimamia ujenzi wa jengo hilo hadi lilipofikia na kuhakikisha linajengwa kwenye ubora unaotakiwa.Maj Gen SM Busungu alimuomba
waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa DR Mwinyi kwenda kuwaombea samani RA ambazo walizitaifisha kutoka bandarini ambazo maarufu kama samani za makonda ili ziweze kutatua changamoto hiyo katika jengo hilo la utawala.

Akijibu ombi hilo la mkuu wa majeshi ya JKT waziri Mwinyi alisema ataenda kuwaomba TRA kwa kuwa wote wanaitumikia serikali moja.

No comments:

Post a Comment