Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga,
Balozi wa China Wang Ke pamoja na viongozi mbalimbali wakikata kike
katika maadhimisho ya miaka 50 kati ya Tanzania na China katika Sekta ya
Afya iliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano
katika sekta ya afya kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika
Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa China nchini Tanzania Wang Ke akizungumza katika sherehe za
maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano katika sekta ya afya kuhusiana na
China kujihusiha katika masuala ya afya pamoja na ujenzi wa Hospitali
uliofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga akizungumza
katika sherehe za maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano katika sekta
ya afya na ushirikiano kati ya Tanzania na China katika masualaya
kidiplomasia , sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Ubalozi wa
China jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed
Janabi akizungumza kuhusiana na mchango wa China katika Taasisi hiyo
katika maadhimisho ya miaka 50 kati ya Tanzania na China katika Sekta ya
Afya yaliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akikabidhi zawadi Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke ikiwa
Serikali ya Tanzania kutambua mchango wa China katika hafla ya sherehe
zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akikabidhi zawadi Naibu Gavana wa Jimbo la Shadong Yuan Lini ikiwa
Serikali ya Tanzania kutambua mchango wa China katika hafla ya sherehe
zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja kati ya Mawaziri pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmad Salim. Picha na Chalila Kibuda
No comments:
Post a Comment