Monday, October 22, 2018

SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA KUJIKITA KATIKA UJASIRIAMALI


Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiteta jambo na mtunzi wa kitabu Maida Waziri


WATANZANIA wametakiwa kuwa na msukumo wa kuthubutu kuanzisha shughuli za ujasiriamali ambazo zitakua na kuleta tija kwake yeye mwenyewe na kwa taifa kwa ujumla.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama katika hotuba iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha ujasiriamali mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa itifaki Aman Christopher akiwaongoza Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulege (katikati) na mtunzi wa kitabu Maida Waziri .
Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisalimiana na mtunzi wa kitabu Maida Waziri katika Red Carpet .
Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulege akiongozana na Maida na waziri na waalikwa wengine wanazuoni Dk Goodluck Urasa (kulia),Godfrey Sembeye na Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu (kushoto) wakiiingia ukumbini tayari kwa uzinduzi .Alisema Serikali inahimiza watu kutumia fursa zilizopo nchini ambazo ni nyingi, kufanya ujasiriamali ili kukuza na kuuendeleza uchumi ambao unahitaji viwanda vidogo vya kati na vikubwa.

Akizungumza kabla ya kuzindua kitabu cha Sauti ya Mjasiriamali: Kesho yako ni uthubutu kilichoandikwa na Mjasiriamali mmliki wa kampuni ya ujenzi ya Ibra Contractors, Naibu waziri Ulega alisema historia ya Maida kama ilivyoelezwa katika kitabu inaweka bayana kwamba wananchi wakithubutu wataweza kuibadili Tanzania kuwa ya viwanda.
Naibu Waziri akiwa katika meza

Wageni wakiwa katika ukumbi wakifuatilia yanayojiri


“Tumeona kupitia wasomi, video iliyooneshwa hapa na hata katika majadiliamoya wanazuoni hakuna njia rahisi ya kufikia mafanikio bali ni kule kuthubutu kuanzisha kitu hata kama huna mtaji “ alisema. Alitaka wananchi kuondokana na uwoga na kutumia raslimali zilizopo kujipambanua na kuupiga vita umaskini.

“ Ukisoma maandishi yake utabaini kwamba wote tunaweza kuwa wajasiriamali kinachotukwamisha ni uwoga wetu wa kuthubutu kama mwenzetu Maida alivyofanya kuanzia kuuza mitumba,kumiliki boti za uvuvi, kuuza maziwa hadi kuwa mkandarasi mwenye sifa hapa nchini “ alisema Ulega. Alisema kwa kuwa ujasiriamali ni chanzo kikuu cha bidhaa na huduma mbalimbali wananchi wanaweza kuufahamu ukweli wa kusonga mbekle kwa kupata maarifa kutoka kwenye kitabu hicho ambacho kinahimiza ujasiriamali endelevu.

Abbysolo akiwa katika hafla akitumbuiza akili ya fedha
Naibu Waziri akiteta jambo na Maida

Kitabu hicho chenye sura 12 kina historia kimegawanyika awamu tatu ya kwanza ikiwa ni wasifu wa Maida waziri, pili mapambano yake ya kujijenga kijasiriamali na tatu kanuni na tabia za mijasirimali.

Naibu Waziri Ulega pamoja na kumpongeza Maida Waziri kushirikisha Watanzania maisha yake kupitia kitabu ili kila anayemwangalia aweze naye kufanya ujasiriamali na kujipatia mbinu na weledi kutoka katika kitabu hicho, atafikisha hoja kwa wenzake kuona namna bora ya kufikisha kitabu hicho kwa wanafunzi ili waelewe ujasiriamali kutoka wakiwa wadogo. Katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho, wanazuoni walipata nafasi ya kukijadili kitabu kwa njia ya mdahalo na washiriki kupata nafasi ya kuuliza maswali.

Dk Donath Olomi akizungumza

Akizungumzia fikira muhimu za kitabu Dk Donath Olomi kutoka taasisi ya IMED alisema kwamba amekuwa mwalimu wa ujasiriamali kwa miaka zaidi ya 30 na katika muda wote huo hajawahi kupata kusoma kitabu chenye uhalisia kama cha Maida waziri kuhusu ujasirimali. Alisema Maida Waziri ameonesha njia ya kwamba katika ujasiriamali unaanza na kile kinachowezekana kama yeye alivyoanza na sh Elfu kumi kununulia mitumba na sasa anamiliki kampuni tano ikiwamo ya ukandarasi ya Ibra Contractors.

Alisema kutokana na kitabu hicho taifa linatakiwa kuona umuhimu wa kuanza kufundisha ujasiriamali katika shule ili kuongeza ufahamu na mbinu za kuushiriki. “Maida amekuwa mwalimu, mtafiti na mshauri mkubwa katika tasnia ya ujasiriamali kupitia kitabu chake akitoa mchango mkubwa katika ajenda ya kujenga ujasirimali nchini “ alisema Dk Olomi.
Dk Goodluck Urasa akizungumza

Naye Dk Goodluck Urassa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alimsifu Maida kwa kuandika kitabu hicho ambacho kina nguvu kubwa kutokana na kuelezea maisha yake na jinsi alivyothubutu katika ujasiriamali. “Vitabu vinaandikwa vya namna mbili. Moja kinaandikwa maisha ya watu wengine kupitia utafiti na kusoma na mbili ni kuandika kitabu kueleza maisha yanayokugusa. Hii aina ya pili ina nguvu kubwa na dada Maida ameweza” alisema Dk Goodluck.

Mtaalamu huyo alisema kitabu kimeeleza na kuonesha kwamba hakuna njia ya mkato katika kukabvili umaskini na kufanya ujasirimali bali ni kuthubutu na kuchukua hatua. Aidha Dk Goodluck alitaka wazazi kuanza kutambua umuhimu wa malezi kwani yanachangia mtu kuwa mbunifu. “Unashangaa mtoto mkubwa katika nyumba hajui wapi alipoweka begi lake la shule dada anaagizwa amtafutie” alisema Dk Goodluck ambaye alisema tabia hiyo inachochea uvivu na udumavu wa maamuzi.
Maida Waziri akizungumza


Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiangalia kitabu baada ya kukizindua

Tabasamu baada ya kazi nzito kitabu kikioneshwa kwa washiriki wa hafla

Naye mtunzi wa Sauti ya Mjasiriamali: Kesho Yako Ni Uthubutu, Maida Waziri amewataka watanzania kuchota maarifa na weledi kutoka kwenye kitabu hicho ambacho kimeelezea historia ya maisha yake na jinsi alivyopambana katika ujasiriamali. Aidha alisema katika kitabu hicho ameeleza sifa za mjasiriamali na kanuni anazostahili kuzifuata ili kuwa na mafanikio.
Naye Mhariri mzalishaji wa magazeti ya serikali Beda Msimbe ambaye alipitia kitabu hicho aliwataka wale wanaopenda kuupiga vita umaskini kuhakikisha kwamba wanakisoma kwa kuwa kimejaa maarifa na kutia moyo.Kitabu hicho kinapatikana kupitia www.maidawaziri.com

No comments:

Post a Comment