Wednesday, September 5, 2018

DC TANGA AZINDUA KAMPENI JUMUISHI YA UPIMAJI WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI MKOANI TANGA

 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mpango wa Furaha Yangu uliokuwa na lengo la Pima,Jitambue ambapo kwa mkoa wa Tanga imezinduliwa leo kwenye viwanja vya Tangamano kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florance Temu 
 Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florance Temu
MKURUGENZI wa Mpango wa Furaha Yangu kutoka Shirika la  Benjamini Mkapa Rahel Sheiza akizungumza katika uzinduzi huo
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu akizungumza katika uzinduzi huo
 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim akizungumza katika uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella anayefuata ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita
 Mwakilishi wa JWTZ akizungumza katika uziunduzi huo
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella   kulia akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha mahita wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo
Sehemu ya wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo kulia ni Suleimani Zumo Afisa Tarafa,nyuma waliokaa aliyevaa miwani ni Afisa Mradi wa Mkoa wa Tanga wa Kifua Kikuu na Ukimwi Dkt Anastazia Masanja
Mgenii rasmi kwenye uzunduzi huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati mwenye koti la suti akikagua mabanda mara baada ya kufanya uzinduzi huo
Mgenii rasmi kwenye uzunduzi huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita
Wasanii wa kundi la Tanga Kwanza wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo

NA MWANDISHI WETU,TANGA.

KATIKA kuendeleza kuchangia juhudi za Serikali kuimarisha huduma za Afya ikiwemo huduma za Ukimwi,Shirika la Benjamini Mkapa kupitia Shirika lisilo la Kiserikali la Amref chini ya ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) inatekeleza mradi wa miaka mitatu 2018-2020 Desemba.

Mradi huo wenye kufanya upimaji Jumuishi wa Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Jamii na Kuhamasisha Jamii kubadili tabia hatarishi ili kuweza kusaidia kupunguza maambukizi hayo kwa jamii .

Hayo yalisemwa na Afisa Mradi wa Mkoa wa Tanga wa Kifua Kikuu na Ukimwi Dkt Anastazia Masanja wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanywa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwenye viwanja vya Tangamano mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita,Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu  na Mkurugenzi wa Mpango wa Furaha Yangu kutoka Shirika la  Benjamini Mkapa Foundation Rahel Sheiza akizungumza katika uzinduzi huo

Alisema kupitia mradi huo wa kupambana na kifua kikuu na Ukimwi ambao utekelezaji wake umeanza mwezi Juni 2018,Taasisi imepewa wilaya mbili ambazo ni Kilindi na Pangani kwa Mkoa wa Tanga .

"Kwa kipindi hiki Shirika la Benjamini Mkapa linatarajia kufikia kata zote 35 ambapo kati ya hizo 21 ni za wilaya ya Kilindi na 14 ni za wilaya ya Pangani lengo la upamaji kwa kila kati ni kuweza kupima watu 2081(Jumla 72,839 kwa kata 35).

Huduma ambazo zimekuwa zikitolewa ni pamoja na uchunguzi wa awali wa kifua kikuu ambapo watu wote 7082 waliohudhuria waliweza kuchunguzwa ambao watu 220 walikutwa na dalili za kifua kikuu na kupewa rufaa kwenda Hospitali ya wilaya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

"Kwa upande wa shinikizo la damu ambapo jumla ya watu 5269 walipimwa kati yao 182 walikutwa na shinikizo la damu lisilokuwa la kawaida "Alisema.

Afisa Mradi huyo alisema pia huduma za uzazi wa mpango zilitolewa ikiwamo vipandikizi,sindano,vidonge ambapo jumla ya wakina mama waliopata huduma hiyo walifikia 188 na ugawaji wa kondomu ambapo jumla ya kondomu 5000 zimegawiwa.

"Lakini pia tuliotoa elimu ya mfuko wa Afya ya Jamii ikiwemo ya mabadiliko ya tabia kupitia sinema na vikundi vya ngoma "Alisema

No comments:

Post a Comment