Friday, August 17, 2018

MAADHIMISHO YA 15 YA SIKU YA WAZAZI BWAWANI SEKONDARI YAFANA MKOANI PWANI

Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP - Phaustine Kasike akisalimiana na mmoja wa wazazi alipowasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Bwawani kushiriki Maadhimisho ya Kumi na tano ya Siku ya wazazi ya Shule hiyo leo Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP - Phaustine Kasike akikagua gwaride maalum lililoandaliwa na wanafunzi skauti wa Shule ya Sekondari Bwawani leo katika Maadhimisho ya Kumi na tano ya Siku ya wazazi ya Shule hiyo, Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anthony Sogoye akitoa maelezo mafupi kabla ya hotuba ya Mgeni rasmi.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP - Phaustine Kasike akitoa hotuba fupi mbele ya wazazi na wanafunzi wa Bwawani Sekondari katika Maadhimisho ya Kumi na tano ya Siku ya wazazi ya Shule hiyo leo Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.
Wanafunzi wa Bwawani wakitoa burudani ya Wimbo Maalum wa Shule hiyo kama inavyoonekana katika picha.
Meza Kuu wakiimba wimbo wa Shule ya Sekondari Bwawani kama wanavyoonekana katika picha(katikati) ni Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP - Phaustine Kasike(kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo ambaye ni Kamishna wa Magereza,Gaston Sanga(kushoto).
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP - Phaustine Kasike akisoma ubao mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa nyumba ya walimu wa Shule ya Sekondari Bwawani leo Siku ya wazazi, Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.
Muonekano wa nyumba ya walimu iliyokamilishwa kujengwa kwa kujitolea tayari kwa matumizi katika Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Bwawani Sekondari wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP - Phaustine Kasike(hayupo pichani) katika Maadhimisho ya Kumi na tano ya Siku ya wazazi ya Shule hiyo leo Agosti 16, 2018 Mkoani Pwani.(Picha na Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment