Meneja wa Pori la Akiba la Litumbandosi, Doreen Lyimo akiwa ameongozana na Naibu Waziri
wa Maliasili alipotembelea Pori la Akiba la Lipalamba kwa ajili ya kuona eneo ambalo wananchi
waliovamia ndani ya hifadhi ya Lipalamba lililopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ikiwa
muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale
na Uendelezaji Utalii.
NA LUSUNGU HELELA- RUVUMA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Wakazi wa Kijiji cha Ndondo kata ya Jangwani wilayani Nyasa mkoani
Ruvuma wamekiri mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kuwa wamevamia na
wanaishi ndani ya eneo la hifadhi ya pori la akiba la Lipalamba lakini kwa kuwa hilo eneo wameshalizoea
wanaiomba serikali kubadilishana nao na eneo jingine la kijiji lenye ukubwa sawa na eneo hilo
walioingia ndani ya hifadhi hiyo.
Wananchi hao wametoa maombi hayo jana kwenye kwenye mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri
huyo alioambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyasa kwa ajili ya kuzungumza na
wananchi wa kijiji hicho kwenye ziara ya siku tatu ambayo Naibu Waziri huyo aliifanya ikiwa ni
muendelezo wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji wenzake, Pancrease Ndunguru alisema kuwa mpaka
unaotenganisha kati ya kijiji na pori hilo ni mto unaojulikana kwa jina Tanginyama lakini wao
wamejikuta wamevamia eneo hilo kwa kuanzisha makazi hivyo wanaomba hiyo sehemu waendelee
kuishi lakini wakubali kubadilishana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndondo waliovamia Pori Akiba la Lipalamba iliyopo wilayani Nyasa moani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.
‘’Hili eneo sisi tushalizoea tunaiomba serikali ikubali ombi letu la kuweza kubadilishana na eneo lingine
nje ya ukubwa sawa na eneo hili Alisema Pancreance Ndunguru.
Naye, Diwani wa eneo hilo Ditram Nchimbi alimsihi Naibu Waziri alifanyie kazi ombi hilo la wanakijii
kwa vile wameonesha uungwana kwa kutambua kuwa wamevamia baadhi ya eneo katika hifadhi ya
Lipalamba lakini kitendo cha kukiri kosa ni uungwana wa hali ya juu hivyo walifanyie kazi ombi lao.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga aliwaambia
wakazi wa eneo hilo kuwa amelisikia ombi lao lakini hata hivyo suala la kubadilishana maeneo hayo na
linaweza likawa sio rahisi kiasi hicho kwa vile sehemu hiyo kuna wanyama adimu aina ya palahala
ambao hawawezi kuhamishika.
Aidha Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa eneo wanalotaka wabadilishane halijajulikana lina ukubwa
kiasi gani na eneo wanalotaka kupewa lina ukubwa kiasi gani.
Kufuatia ombi hilo, Naibu Waziri huyo alisema kuwa watatuma wataalamu wenye ujuzi wa ikolojia ili
kuja kutafiti ya maeneo hayo baaada ya ripoti hiyo ya wataalamu kukamilika ndipo maamuzi yataweza
kufanyika.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndondo kata ya jangwani mara baada ya kupewa zawadi ya gunia la mahindi na mbuzi mmoja akiwa yeye kiongozi wa kwanza wa juu kuwatembelea na kuzungumza nao lakini hata hivyo zawadi hizo aligawa kwa ungozi wa shule ya msingi ya Ndondo kwa ajili ya kuwapa chakula wanafunzi .
Aidha, aliongeza kuwa kwa kuwa Wizara ya ardhi ndio wenye dhamana ya kusoma ramani, hivyo
wataiomba Wizara hiyo iweze kutuma watalamu kwa ajili ya kusoma ramani
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo alipiga marufuku kwa mwanakijiji yeyote kuingia katika eneo
hilo lenye mgogoro kati ya wananchi na serikali kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo mpaka pale
maamuzi yatakapofanyikiwa.
Pori la akiba la Lipalamba linalomilikiwa na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania TAWA ina ukubwa na ni
hifadhi mpya yenye ukubwa wa kilomita za mraba liko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Awali Mkuu wilaya hiyo, Elizabeth Chilambo aliwataka wananchi hao kuwa mstari wa mbele kwa
kuwafichua wanakijiji wenzao wanaojihusisha na ujangili na vitendo vya ujangili.
Katika hatua nyingine, Wakazi wa eneo hilo mara baada ya mkutano kuisha , walitoa zawadi ya gunia la
mahindi pamoja na mbuzi ikiwa ni ishara ya kuonesha kufurahishwa na uamuzi wa kutembelea kijiji
hicho kwa vile tangu kuanzishwa kwake hakuna kiongozi yeyote mkubwa aliyewahi kukanyaga katika
hata hivyo baada ya kukabidhiwa zawadhi hzo naye alitoa zawadi kwa shule ya msingi ya Ndondo ili
wanafunzi waweze kula wakienda shule.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndondo kata ya jangwani mara baada ya kupewa zawadi ya gunia la mahindi na samaki wakati alipotembelea kwa ajili ya kuzungumza wananchi waliohamia ndani ya hifadhi ya Lipalamba iliyopo wilayani Nyasa moani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akioneshwa eneo la Pori Akiba la Lipalamba kutoka kwa Meneja wa Pla akiba la Lipalamba , Ramadhan Isomanga wakati alipotenbelea Pori hilo lililopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndondo kata ya jangwani wakati alipotembelea kwa ajili ya kuwasilikiliza wananchi hao waliovamia Pori hilo lililopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.
No comments:
Post a Comment