Monday, June 25, 2018

WATAALAM WA BIMA NCHINI WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI, KUBUNI BIDHAA MPYA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WADAU na wataalam wa masuala ya Bima nchini wameshauriwa kufanya kazi kwa weledi,kujiheshimu na kubuni bidhaa mpya na za bei nafuu ili kuwafikia wananchi wote.

Ushauri huo umetolewa jana na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Bima Nchini (TIRA)Dk. Baghayo Saqware wakati akiwahutubia wanafunzi wanaosoma kozi ya Bima katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mara baada ya matembezi ya utambuzi wa Bima yaliyoanzia katika viunga vya IFM hadi Karimjee.

"Watoa huduma za bima nchini lazima tuwe na wajihi au taswira njema kwa jamii inayo tuzunguka ,kwani jamii hiyo ndiyo walaji wa bidhaa za bima."Hivyo basi hatunabudi kujiheshimu na hatupaswi kuonekana matapeli,wahuni. Tuoneshe heshima mbele za wananchi wote ili wawe na uthuubutu wa kuwa na bima,” amesema Dk Saqware.

Amewataka wataalamu wa bima kuwa wabunifu kwa kubuni bidhaa mbalimbali na kuongeza ufahamu wa bima kwa wananchi kwani bima ni kinga na bima ni muhimu kwa kila mwananchi kuwa nayo kwa ajili mali na maisha.Mkuu wa Idara ya wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dk. Mussa Juma amesema IFM kila mwaka hufanya matembezi hayo kwa lengo la kujenga uwelewa kwa wananchi wajuwe umuhimu wa bima katika kuweka kinga ya mali na maisha.

Amesema matembezi yao ni kuwaelimisha wananchi ikiwa kwa kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kutoa vipeperushi kwa mtu mmoja mmoja pamoja kueleza aina za bima zinazopatikana kwa bei nafuu ili wananchi wa kipato cha chini waweze kumudu.Aidha Dk. Juma amesema kuna changamoto ya wataalamu wa bima na kuongeza pamoja na changamoto za uchache huo bado wanajitahidi kuwafikia wananchi kwa kadri wawezavyo.

Hata hivyo Sekta hiyo inakumbwa na changamoto ya uwelewa mdogo kwani watu wengi hawajui umuhimu wa bima, hivyo lazima jitihada za msingi zifanyike.
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Bima Nchini (TIRA) Dk. Baghayo Saqware akizungumza wanafunzi wa Chuo cha IFM wanaosoma masuala ya bima baada ya kufanya matembezi ya kuhamasisha wananchi kujua umuhimu wa bima.
Mkuu wa Idara ya wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dk Mussa Juma akizungumza kuhusiana na Chuo kilivyojipanga katika utoaji elimu ya bima kwa vijana na wanaohitaji kutokana na kuwa na soko kubwa la ajira.
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anaesomea Bima ,Mkagambage Kyaruzi akizungumza na waandishi kitu ambacho kimemsukuma kusomea bima . 
Matembezi ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Mawakala wa Bima
Matembezi ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Mawakala wa Bima
Matembezi ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Mawakala wa Bima

No comments:

Post a Comment