Monday, June 25, 2018

WAKULIMA 11,177 WA UFUTA WANUFAIKA NA MRADI WA FARM AFRIKA-DKT TIZEBA

Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam

Utekelezaji wa mradi wa Farm Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu umeweza kuwafikia wakulima takribani 11,177 ambapo kati yao wanawake ni 5,474 na wanaume ni 5,703 huku kati ya wakulima hao vijana wakiwa ni takribani 5,821 yaani zaidi ya nusu (52%) kutoka wilaya ya Bahi, Manyoni na Babati.

Hayo yamebainishwa juzi 22 Juni 2018 na Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam.

Dkt Tizeba alipongeza jitihada hizo kwani zinachangia kukuza kipato cha wakulima na uchumi wa nchi kwa kuingiza fedha za kigeni huku akiwataka watumishi mbalimbali kuwaunganisha wakulima wadogo wadogo katika masoko rasmi na kujenga uelewa wao juu ya vichocheo na fursa za ushiriki endelevu.

Waziri huyo wa kilimo alilishukuru shirika la Farm Afrika kwa kuona umuhimu na fursa zilizopo katika kilimo cha ufuta katika mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara hivyo kuwanufaisha wakulima kupitia mbinu bora za kilimo cha kisasa katika zao hilo.

Alisisitiza kuwa zao la ufuta lina fursa kubwa ya soko ambapo kwa sasa mahitaji ya soko ni zaidi ya mara tatu ya kiasi kinachozalishwa kwa mwaka ambapo hali hiyo inatokana na nafasi kubwa kwa wakulima wa ufuta kujipatia kipato na kuboresha maisha yao.

Alisema kuwa serikali inaweka mkazo mkubwa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta na juhudi hizo zinajidhihirisha katika hatua ambazo serikali inaendelea kuzichukua kwa kuhakikisha uzalishaji wa mbegu za mafuta ndani ya nchi unaongezeka.

Alisema, kupitia utekelezaji wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili mbegu za mafuta ikiwa ni pamoja na ufuta na alizeti ni miongoni mwa mazao ya kipaumbele ambapo kwa kuanzia msimu wa mavuno ujao zao la ufuta litaingizwa kwenye mfumo wa stakabadhi za ghala na katika kuimarisha upatikanaji wa soko la ziada kwa zao la ufuta na mbegu nyingine za mafuta, Na kuongeza kuwa Bodi ya mazao mchanganyiko kuanza kununua mazao hayo ili kuhakikisha mkulima anapata soko la uhakika zaidi.

Katika hatua nyingine, Mhe Dkt Tizeba aliwasihi wakulima wa ufuta kote nchini kubadilika kuanza kufanya kilimo biashara na kuachana na kilimo cha mazoea cha kujikimu ikiwa ni pamoja na kujua mahitaji ya soko kwa maana ya ubora wa ufuta na kiasi, kutumia teknolojia hususani zana bora, mbegu bora na mbolea sambamba na kujiunga katika vikundi au ushirika na kuuza kwa pamoja na kuwa na nguvu ya pamoja.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Farm Afrika Ndg Ryan Whalen akizungumza wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018. 
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.
Baadhi ya wadu waliohudhuria mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.

No comments:

Post a Comment