Tuesday, June 26, 2018

RC TABORA AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KWA WATENDAJI WALIOSABABISHA KUWEPO HOJA ZA CAG

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri(mwenye Kaunda suti) na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri(kulia) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Bundala Kiwele (kushoto) wakibadilishana mawazo wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri akitoa maoni wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Robert Makungu akitoa maoni yake wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoani Tabora kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Mohamed Msangi alitoa taarifa ya ukaguzi wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakiwa katika Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Jacob Mtalitinya akitoa ufafanuzi wakati Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupulla akitoa ufafanuzi wakati Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameuagiza Katibu Tawala Mkoa (RAS) kuwachukuliwa hatua Wakuu wa Idara wote waliosababisha kuibuka kwa hoja za ukaguzi wa Hesabu za serikali katika Halmashauri mkoani humo.

Aliyasema hayo jana wilayani Nzega kwenye baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo la kujadili na kujibu hoja za Mkaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu.

Mwanri aliwataka RAS kuanza kuwachukulia hatua kwa kuwaondoa Wakuu wote wa Idara ambao wamekwenda kinyume cha taratibu na hivyo kuzisababishia Halmashauri zao kuwa na hoja.

Alisema hoja nyingi ambazo zimeibuka zinasababishwa na wakati mwingine manunuzi yaliyofanyika kukosa viambatanisho kama vile stakabadhi za malipo yaliyofanyika na nyingine kutofuata taratibu za manunuzi jambo ambalo linaloelekea katika matumizi mabaya ya fedha za umma.Mwanri alisema Serikali haiwezi kumvumilia Mtendaji au Mkuu yoyote wa Idara ambaye hana nidhafu katika matumizi ya fedha za umma na hivyo kusababisha hasara ambayo inapelekea baadhi ya miradi kutokamilika.

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa Mwezi mmoja hoja zote zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali zinapata majibu ikiwa na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kusababishia Halmashauri ya Wilaya ya Nzega hasara.Alimwagiza Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha kwa wale ambao walisababisha hasara Halmashauri hiyo kuwasiliana na Tamisemi hata kama wamehama warudishwe waje wajibu hoja zinazowakabili.

Katika hatua nyingine aliitaka Halmashauri hiyo kuja na utaratibu wa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na ile asilimia 10 kwa ajili ya vijana , wanawake na walemavu.Alisema kuwa utaratibu huo ni lazima pia uonyesha jinsi pesa hizo zitakavyorejeshwa ili watu wengine waweze kukopa.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Robert Makungu aliwataka watendaji mbalimbali kuwa na uzalendo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha kila wanachokifanya kinazingatia maslahi mapana ya umma.

Alisema moyo wa kizalendo ndio utasaidia kukwepa dosari mbalimbali zinazoibua hoja kutoka kwa Mkaguzi wa hesabu za serikali.Aidha aliwataka Wadiwani na Watendaji kufanyakazi kwa ushirikiano katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Akiwasilisha taarifa ya CAG inayohusu Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Tabora Mohamed Msangi alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 zilitolewa hoja 40 ambapo kati ya hizo 14 zimefungwa na hoja 26 zimesalia.

No comments:

Post a Comment