Tuesday, May 8, 2018

WASATU ILIVYOVIMBA BIRMINGHAM , UINGEREZA KUSAIDIA VIGOLI BONGO, APRIL 28

PICHA NA HABARI Za Freddy Macha 3-bango la WASATU 

 Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini, Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. 
Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula , sanaa usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru. WASATU iliyoundwa mwaka 2016 chini ya udhamini wa Balozi, Uingereza, Mhe Asha Rose Migiro, inakutanisha wasanii wa ala mbalimbali chini ya viongozi- mwanamuziki na mcheza sarakasi mwenye nidhamu ya hali yajuu, Fab Moses na mtangaza mapishi ya Kitanzania, Uingereza, Bi Neema Kitilya, aliyetulizana kama shingo ya twiga....Mwaka jana, 2017, shughuli hii ilifanywa Northampton na asilimia 20 ya kipato iliwafikia Watanzania waliofikwa na maafa ya mafuriko ya maji. 2- Warembo walioonesha mavazi ya Kitanzania- pic by F Macha 2018 Warembo wa kujitolea, walioonesha mavazi yaliyoandaliwa na kampuni ya “All Things African” (inayoendeshwa na Mtanzania, mchapa kazi, asiyejua uvivu kabila gani, Hamida Mbaga). Toka kushoto, Yvonne Waweru, Georgeous Katega, Victoire Koleilas, Maureen Tibenda 3-Viongozi wa WASATU -Neema Kitilya na Fab Moses wakijadiliana -p;ic by F Macha 2018 Viongozi wa WASATU – Neema Kitilya na Fab Moses wakijadiliana huku shughuli zikikwea minazi, miguu na kuta. 4- Tanzania Yetu- pic by F Macha 2018 Fahari ya Tanzania – imesambazwa meza ya bidhaa mseto ya “All Things African” inayoendeshwa na Hamida Mbaga aliyesafiri toka Manchester. 5- Likiwa Ismail akionesha SINDIMBA- pic by F Macha 2018 Mcheza ngoma aliyepitia mitihani mikali na vikundi maarufu vya mila zetu- Kibisa na Muungano - Likiwa Ismail- akionesha SINDIMBA – bila aibu, staha wala wasiwasi. 6- Baadhi ya vyakula - pic by F Macha 2016 Baadhi ya vyakula vya Kitanzania 7. 7- Ramasax akipuliza vituz- pic by F Macha 2018 
 Rama Sax akipuliza vitu. Zamani alipiga na Simba Wanyika akashiriki kurekodi wimbo wa “Sina Makosa”. Rama Sax ni pia mwimbaji mahiri 8- Neema John aliyetengeneza misosi akionsha Salad- pic by F Macha 2018 
 Msanii wa mapishi Neema John aliyechangia kazi njema na Neema Kitilya. 9-Wageni toka Tanzania na Uganda Wageni toka Tanzania na Uganda. Huyo Mganda (kushoto) ni mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili 10- MPiga gitaa Jioni TIcha na Mkuu wa Kuku Mpiga Gitaa mkuu wa shughuli, Jioni Ticha na kipande cha kuku baada ya jasho kali jukwaani. Alisafiri toka Leeds. Mbali si haba na hapa... 11- Watanzania wakichangamka Watanzania wakichangamkia tafrija ya msanii adilifu wa Kitanzania 12- Sia Travel akihamasika Sia Travel akihamasika. 13- Mwanamuziki Saidi Kanda akiwa na Watanzania Mwanamuziki Saidi Kanda,(aliyesimama) mtukuzaji vyombo asilia vya muziki wa Kitanzania, akijumuika na Wabongo nadhif, waliokuwemo 14- F Macha, ikiwa Ismail na Rama SaxMwandishi na mtunzi, Freddy  Macha pamoja na Likiwa Ismail (ngoma) na Rama Sax.

No comments:

Post a Comment