Monday, May 28, 2018

RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua majengo ya shule ya Chagongwe wakati wa ziaya yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kushoto) wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kumaliza ufunguzi wa majengo ya shule ya sekondari Chagongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chagongwe waliojitokeza kumpokea wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Gairo na vitongoji vyake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akimsikiliza mmoja ya wazee waliojitolea eneo la shamba lake kwa ajili ya kujenga sekondari ya Chagongwe ambapo alitoa eneo la heka 25.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipewa zawadi ya mbuzi na Diwani wa Kata ya Chagongwe mara baada ya kuwa amemaliza kuwahutubia wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakionyeshwa eneo la shule ya Nongwe lililovamiwa na wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua vyoo vya hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakishiriki ngoma wakati wa mapokezi yao katika shule ya sekondari Nongwe.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) akiwasalimia wananchi wa Kijiji Cha Nongwe waliohudhuria katika mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili kijijini kukagua miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwahutubia wananchi wa Kijijini Nongwe waliohudhuria katika mkutano wa hadhara.
Burudani ya ngoma ikiendelea.
Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya kukagua maendeleo katika wilaya ya Gairo. Hapa alikuwa akielekea Kata ya Kata ya Chagongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe)  akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakikagua ubovu wa barabara ya Chagongwe ambayo kwasasa imeharibika kutokana na mvua inayoendelea kunyesha maeneo mbali mbali.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe wakikagua Daraja la Barabara ya Chagongwe-Kumbulu yenye urefu wa Km 34 lililojengwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kulia) wakiongozwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) kukagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa katikati) wakipewa maelezo machache na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) kukagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kulia) wakipewa maelezo machache na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) wakati wakikagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA. Pembeni ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya (aliyejifunika shuka).
Msafara ukiondoka Darajani.
Mmoja ya wazazi akitoa elimu ya jinsia kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Chagongwe. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo. 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameuagiza uongozi wa wilaya ya Gairo na mkoa wetu kwa ujumla kuhakikisha wanafunzi wa shule msingi mpaka sekondani wanapatiwa chakula mashuleni. Kauli hiyo ameitoa wishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika Ufunguzi wa madarasa ya shule ya sekondari Chagongwe katika ziara yake kwa siku ya tatu Wilayani Gairo kukagua miradi ya maendeleo.

 Ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Gairo kujiwekea mpango kazi ili kuwawezesha watoto wote kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari wanapatiwa chakula cha mchana na kuwawezesha waweze kufanya vizuri katika masomo yao. "Watoto wa shule za Morogoro kutokula chakula mashuleni ni aibu, sitaki kabisa kusikia hili suala watoto kunyimwa chakula, naomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo, upitishe azimio kwenye baraza na shule ambayo hawatatoa chakula shuleni wachukuliwe hatua uongozi wa eneo hilo," amesema Dkt. Kebwe.

 "Mkoa wetu unaongozwa kwa uzalishaji wa chakula cha kutosha sasa inakuwaje watoto wetu tuwanyime chakula, tutakosa matokeo mazuri," amesema.Aidha amesema kuwa mtoto anatakiwa kula chakula mara mbili ya mtu mzima, unapomnyima chakula hata ukuaji wake unakuwa hafifu... "Ubongo unatakiwa kupata chakula gram 6 za grucose" Amesema kuwa kukosekana kwa chakula shuleni kumekuwa kukichangia matokeo mabaya kwa wanafunzi bila kujali ni shule ya msingi au sekondari.

 "Tatizo hili tulilizungumza wakati tunafanya tathimini ya mkoa juu ya kushuka kwa elimu na jambo lililojitokeza ni wakafunzi kutopewa chakula kunachangia matokea mabaya" amesema. Alisisitiza kuwa Halmashauri zote zisimamie suala la chakula shuleni ni lazima na wala siyo hiari naomba uongozi usimamie kwa msisistizo mkubwa, kuanzia walimu wakuu, wakuu wa shule atakula nao sahani moja na akiona ni waheshimiwa madiwani ndiyo hawahamasishi atabanana nao mpaka kieleweke. 

"Mwaka juzi tulikuwa tunashika mkia nafasi ya 23 katika upande wa matokeo ya elimu, ila tokea tulipoanza kubanana vizuri matokeo yameonekana mpaka sasa tupo nafasi ya 11 kitaifa ni jambo linaloleta faraja sana, Kidato cha sita tunaongoza maana tupo nafasi ya pili kitaifa, sekondari tumesogea mpaka namba 14 kitaifa" amesema. 

Ameongeza kuwa tamko lake hilo lisije kutafsiriwa vibaya kuwa tunawatoza michango ya hela, michango haipo kwa waraka namba 6 umefafanua elimu bila malipo, tatizo lenu wengine wanasema  elimu bure, hakuna elimu ya bure ni elimu bila malipo kwa mzazi ila serikali ndiyo inagharamia. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe amemshukuru Mkuu hiyo kwa kutenga muda wake na kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo na kumhaidi kufanyia kazi changamoto na maelekezo yote aliyoyatoa.

 "Mkuu wa Mkoa tunakushukuru sana kwa kuweza kufika eneo letu na kuona changamoto tulizo nazo tunahidi kuzifanyia kazi na tunakuomba ufikishe salamu zetu pia kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuikumbuka wilaya yetu kwa kutupa hela za maendeleo," Mhe. Siriel amewaomba vingozi wa wilaya ya Gairo kuendeleza upendo na mshikamano walionao ili kuendelea kuwatumikia wananchi vyema.

No comments:

Post a Comment