Thursday, May 3, 2018

RAIS MAGUFULI,MBUNGE MAVUNDE NA DC NDEJEMBI WATIMIZA AHADI YAO YA KUCHANGIA SHULE YA MSINGI VEYULA-JIJINI DODOMA

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki kuchimba msingi wa ujenzi wa madarasa shule ya msingi Veyula.

 Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki kuchimba msingi wa ujenzi wa madarasa shule ya msingi Veyula pamoja na wananchi.
 Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akimkabidhi fedha Kaimu Mkuu wa wilaya wa Dodoma Deogratias Ndejembi ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Veyula(katikati) ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akimkabidhi saruji Kaimu Mkuu wa wilaya wa Dodoma Deogratias Ndejembi ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Veyula.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki ushushaji mifuko ya sarufi
Kaimu Mkuu wa wilaya wa Dodoma Deogratias Ndejembi akizungumza na wananchi kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Veyula.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungunza.
Wananchi walioshiriki uchimbaji msingi
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde na Kaimu Mkuu wa wilaya wa Dodoma Deogratias Ndejembi.
Kaimu Mkuu wa wilaya wa Dodoma Deogratias Ndejembi akichimba msingi vyumba vya madarasa shule ya msingi Veyula.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi

...............................................................
Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli leo amewasilisha mchango wake wa  10,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Veyula iliyopo Jijini Dodoma ikiwa ni ahadi aliyoitoa kwa wananchi  wakati aliposimama kuwasilimia akitokea katika hafla ya Ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati.

Mchango huo umewasilishwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Deogratious Ndejembi ambaye pia amechangia Tsh 1,000,000 kutimiza ahadi yake na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuanza kuchimba Msingi wa ujenzi wa madarasa na kutumia fursa hiyo kuwataka watendaji wote kusimamia zoezi la ujenzi kwa ufanisi na kumwagiza Lt Col Matina Mkuu wa Kikosi cha JKT Makutupora kusimamia ukamilishwaji wa ujenzi wa madarasa hayo ndani ya wiki tatu.

Aidha,Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde na DC Ndejembi waliungana na wananchi katika zoezi la uchimbaji msingi na baadaye Mh Mavunde alikabidhi kiasi cha Tsh 5,000,000  mifuko ya Saruji 100 na kuahidi kuongeza Tsh 5,000,000 ya ziada mapema wiki ijayo ikiwa ni mchango kutoka kwa marafiki wa Mbunge huyo,na pia alitumia fursa hiyo kumshukuru Mh Rais kwa kusaidia ujenzi wa madarasa hayo.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewahakikishia wananchi kwamba Halmashauri ya Jiji la Dodoma italipia vifaa na gharama zote za kupaua madarasa hayo ikiwa ni sehemu ya mchango wa Jiji.

No comments:

Post a Comment