Saturday, May 12, 2018

PRECISION AIR YAPANDA MITI ELFU MOJA MLIMA KILIMANJARO


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shirika la Ndege linaloongoza Tanzania, Precision Air, limeshiriki katika jitihada za kuhifadhi mazingira katika maeneo ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Katika kutimiza zoezi hilo, wafanyakazi wa shirikika hilo wakishirikiana na wanakijiji wa kijiji cha Ngarony pamoja na wafanyakazi wa wilaya ya siha wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Siha Valerian Juwal wamefanikishaa upandwaji wa miti 1000 (elfu moja) katika eneo linalotenganisha kijiji cha Ngarony na hifadhi ya mlima Kilimanjaro.

Akizungumzia tukio hilo Meneja Masoko na Mawasiliano wa Precision Air Hillary Mremi amesema, Precision Air inatambua inawajibu wa kutunza mlima Kilimanjaro kwani mlima huo una mchango wa moja kwa moja katika shughulli za shirika hilo. 

“Mlima Kilimanjaro unatutunza vyema sisi kama shirika na kama taifa kupitia utalii, hivyo sote tunawajibu wa kuutunza mlima huu na mazingira kwa ujumla wake.” Mremi alisema.

Precision Air imekua ikifanya safari zake ndani ya mkoa wa  Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka ishirini na nne (24) na kama mdau mmojawapo wa utalii, limefanya zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni moja ya jitihada zake za kuhakikisha jamii inayo uzunguka mlima inaendelea kufaidika na uwepo wa mlima, ambao ni moja ya kivutio muhimu cha utalii nchini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Siha Valerian Juwal amesema kuwa Shirika la Ndege  la Precision Air limeonyesha mfano wa kuigwa na wadau wengine wa mazingira na utalii. Na ameongeza kuwa ni wakati sasa wa kuchukua hatua madhubuti kulinda mazingira yetu ili vizazi vijavyo viweze kufaidika na uzuri wa nchi yetu wa vivutio kama mlima Kilimanjaro na vingine.
Afisa Maliasili wa Kata ya Siha Lazaro Mwaluko amesema kuwa Precision Air wamefanya jambo zuri katika tasma nzima ua uhifadhi mazingira pamoja na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali na wananchi kwenye uhifadhi wa msitu huo.
Mwaluko ameongezea na kusema msitu huo umeweza kuwanufaisha wanakijiji kwa kupewa mizinga ya nyuki ma serikali ambapo tayari imefika 290 na ipo karibuni kuzinduliwa.
Mlima Kilimanjaro  ndio mlima mrefu zaidi barani Afrika, ukiwa na urefu wa takribani mita 5,895 kutoka katika usawa wa bahari, pia ndio mlima mrefu zaidi duniani uliosimama wenyewe (Bila kutegemea kanda za milima).  
Shirika la Ndege la Precision Air lilianzishwa mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi, likifanya safari zake kusafirisha watalii katika vivutio vya utalii kama Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro pamoja na Visiwa vya Zanzibar. Sasa Shirika hilo lenye makoa yake makuu katika Jiji la Dar es Salaam limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika yanayo heshimika katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.Ikifanya safari zake kutokea Dar es Salaam, Arusha, Bukoba, Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza, Tabora, Kahama, Zanzibar,Nairobi na Entebbe.
Wafanyakazi wa Precision Air wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza zoezi la kupanda  miti 1000 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Msitu ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Mkoani Kilimanjaro.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Precision Air Hillary Mremi  akisaini kitabi cha wageni katika ofisi ya Kata ya Siha.

Afisa Maliasili wa Kata ya Siha Lazaro Mwaluko akizungumza na wanakijiji wa Kijiji cha Ngarony wakati wa uoteshaji miti kwenye Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Mlima Kilomanjaro (KINAPA) Mkoa wa Kilimanjaro, kushoto Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Rivishi Ernest Munuo.
 Meneja Masoko na Mawasiliano Hillary Mremi akizungumza na wanakijiji wa Kijiji cha Ngarony wakati wa uoteshaji miti kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)Mkoani Kilimanjaro.
 Meneja Masoko na Mawasiliano Hillart Mremi pamoja na Afisa Maliasili wa Kata ya Siha Lazaro Mwaluko wakiotesha mti kandokando ya mto uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Mlima Kilimanjaro.

 Wanakijiji wa Kijiji cha Ngarony kata ya Siha wakiotesha miti kwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Precision Air katika Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Mlima Kilimanjaro (KINAPA) katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu.
 Wafanyakazi wa ndege wa Precision Air wakiwa katika picha ya pamoja na wanakijiji mara baada ya kutoka kupanda  miti 1000 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Msitu ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngarony Wilson Mmari akizungumza na wanakijiji waliojitokeza katika uoteshaji wa miti kwenye kando ya mto unaopita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Mlima Kilimanjaro (KINAPA) katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu pamoja na kuzuia mmonyoko wa udongo.

Haikuwa kazi rahisi, watu walipambana kushuka mlima na kupanda huku changamoto ya hali ya hewa ikichangia kwa kiasi kikubwa watu kuteleza na hata kuchafuka.
 
Mwana Globu ya Jamii Zainab Nyamka naye aliweza kuotesha mti kuunga mkono jitihada za Precision Air kutunza mazingira ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.
Picha Zote na Zainab Nyamka Globu ya Jamii.



No comments:

Post a Comment