Tuesday, May 8, 2018

Mkazi wa Zanzibar ashinda bidhaa zenye thamani ya Tsh. milioni 1 kutoka Jumia

Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo amejishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili. 

Mshindi huyo alipatikana kupitia kampeni iliyoendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Wateja walitakiwa kupendekeza mtu wao wa karibu ambaye waliona anastahili nyumba yake kupendezeshwa na Jumia kwa kupatiwa ofa ya vyombo vya ndani.

Bi. Patricia Philipo aliibuka mshindi baada ya mchumba wake Bw. Mwalim Juma Kumpendekeza ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.

“Mimi ni mteja mzuri wa Jumia kwa sababu naitumia mara kwa mara kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa zikinifika mpaka ninakoishi Zanzibar. Baada ya kuliona hili shindano, niliona ni vema nimpendekeze mwenzangu ashinde. Ukizingatia tupo kwenye maandalizi ya ndoa yetu, suala la mahari pamoja na vyombo vya ndani ni gharama hivyo ushindi wake ungekuwa na mchango mkubwa kwenye shughuli yetu,” alisema Bw. Juma ambaye ni mchumba wa mshindi wa kampeni hiyo, Bi. Patricia.

“Sikuwa na wasiwasi kwamba endapo angeshinda asingeweza kupatiwa zawadi zake. Kwa sababu hapo nyuma kulikuwa na mashindano kadhaa kama vile ‘Treasure Hunt’ kipindi cha Mobile Week, wateja walikuwa wanashinda simu na kukabidhiwa bila ya ubabaishaji wowote,” alimalizia Bw. Juma.

Akielezea furaha yake mara baada ya kutangazwa mshindi Bi. Patricia Philipo amesema kuwa, “kusema ukweli hapo mwanzo sikutarajia kama ningeweza kushinda kutokana na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wangu. Kuna wakati nilitaka kukata tamaa kwa sababu mwenzangu alikuwa ameniacha mbali, mashabiki wake walikuwa wanamuunga mkono na kuwashirikisha wengine kwa kiasi kikubwa.”

“Lakini niliongeza bidii na kumuomba Mungu ili niweze kufanikiwa. Na kweli ilifika mahala mpinzani wangu akakata tamaa. Hapo ndipo mimi nilipoongeza bidii zaidi na kufanikiwa kuibuka mshindi,” aliongezea Bi. Patricia na kuhitimisha, “nina furaha kubwa katika kipindi hiki kwani zawadi niliyoshinda ni kubwa. Vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja si jambo la kawaida. Jumia wameweka alama kubwa katika maisha yangu na nawaombea waendelee kuwajali wateja wao kwa bidhaa bora, ofa lukuki pamoja na kuwa waaminifu.”

Kampeni ya ‘Big Home Makeover’ kutoka Jumia ilyodumu kwa takribani mwezi mmoja, ilikuwa na dhamira ya kuwawezesha wateja wake kununua vyombo vya ndani kwa gharama nafuu. Lakini pia ilitoa fursa ya kumzawadia mteja mmoja aliyependekezwa na mtu wake wa karibu vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni mmoja.

“Tunampongeza mshindi wetu Bi. Patricia kwa ushindi aliojipatia lakini pia tunawasihi wateja wetu kuchangamkia bidhaa mbalimbali kwenye mtandao wetu. Kupitia mtandao unaweza kuokoa muda na gharama pamoja na usumbufu wa kufuata bidhaa. Lakini cha muhimu ni njia salama na ya uhakika, Jumia inawapatia fursa wateja wake kufanya manunuzi na kisha kulipia baada ya kuridhika na mzigo aliofikishiwa,” alisema Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey.

“Hivi sasa kupitia mtandao wetu tunaendesha kampeni ya kutoa punguzo kubwa la bei ambalo hauwezi kupata sehemu yoyote. Kwa mfano, simu zinazouzwa Jumia ni pungufu ya shilingi 50,000 tofauti na ukienda kwenye maduka moja kwa moja, vivyo hivyo kwa bidhaa nyinginezo, kila bidhaa utakayoiona basi ujue imepunguzwa kiasi hicho! Tunawasihi watanzania wasicheze mbali na jumia ili kuweza kunufaika na mambo haya mazuri,” alihitimisha Geofrey. 
Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni moja,Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo mara baada ya kujishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili.

Bi. Patricia Philipo aliibuka mshindi baada ya mchumba wake Bw. Mwalim Juma Kumpendekeza ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.  
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akizungumza mapema leo jijini Dar kuhusu ushindi wa Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo (hayupo pichani) aliyejishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili.Pichani kushoto ni Mchumba wa mshindi,Bw. Mwalim Juma. 



Mshindi huyo alipatikana kupitia kampeni iliyoendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Wateja walitakiwa kupendekeza mtu wao wa karibu ambaye waliona anastahili nyumba yake kupendezeshwa na Jumia kwa kupatiwa ofa ya vyombo vya ndani.

 Afisa Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Hadija Natalia Tuwano pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey wakimsikiliza kwa makini Mchumba wa mshindi,Bw. Mwalim Juma  akitoa ushuhuda wa namna alivyompendekeza Mchumba wake na kujishindia vyombo vya ndani  mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,Mwalimu Juma  alimpendekeza mchumba wake Bi. Patricia Philipo ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.

No comments:

Post a Comment