Friday, April 20, 2018

TUCTA MEI MOSI 2018 NI HESHIMA KUBWA KWA MKOA WA IRINGA - RC MASENZA

Na  MatukiodaimaBlog

WAKATI  maadhimisho ya  siku  ya  wafanyakazi duniani  kwa  nchini  Tanzania  yaliyoandaliwa na  shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) yakitaraji  kufanyika  mkoani  Iringa   kitaifa  mkuu   wa mkoa  wa Iringa  Amina  Masenza  amesema  mkoa  wa Iringa  kuwa  mwenyeji wa  mei  mosi ni  heshima  kubwa katika  Taifa .

 Akizungumza  na  wanahabari  leo  ofisini kwake    kuhusiana na maandalizi ya  Mei  Mosi  Kitaifa  alisema  kuwa  mkoa  wa  Iringa  umeteuliwa  kuwa mwenyeji  wa maadhimisho hayo  ambapo  mgeni  rasmi atakuwa  ni  Rais  Dkt  John Magufuli .

Alisema  kuwa katika  maadhimisho hayo ya  Mei  Mosi  kitaifa  kauli   mbiu  ni Kuunganishwa kwa  mifuko ya hifadhi ya  jamii kulenge  kuboresha mafao ya  wafanyakazi  na  kuwa  kupitia maadhimisho hayo wakazi  wa  mkoa wa  Iringa na  wafanyabiashara  watapata   fursa  kubwa  ya  kujitangaza  pamoja na  kuonyesha shughuli  zao.

Katika maadhimisho hayo  ambayo   kilele  chake  kitafanyika  uwanja  wa Samora  mjini Iringa  kabla ya  kilele  kutakuwa na  michezo mbali  mbali  kama mpira wa miguu, kuvuta kamba ,bonanza la  michezo  tofauti  ,mpira wa pete ambayo yote yameanza toka  April  17 hadi  April  30 mwaka   huu .

Hata  hivyo  mkuu  huyo wa mkoa   wa Iringa mwenyeji wa  Mei  mosi kitaifa  mwaka  2018  Bi Amina Masenza alisema  sherehe  hizo zitahusisha  maonyesho  ya  shughuli ,huduma na  bidhaa mbali mbali  za wafanyakazi ,taasisi  za  umma na  binafsi ,wawekezaji  na wajasiliamali  zitakazofanyika  uwanja  wa Kichangani  Kihesa  mjini  hapa .

Hata  hivyo  alisema  kwa ajili ya  kuufanya mkoa wa Iringa  uzidi  kuwa fursa kwa  wageni  kutembelea  vivutio  vya  utalii kama  hifadhi ya  Ruaha  na vingine   serikali  imekaa na  wafanyabiashara  wa  nyumba  za  kulala wageni na  Hoteli  ili  kuepuka  kutumia mei  mosi  kupandisha   gharama  za  vyumba  kwa wagen

Bi  Masenza  amewataka   wananchi wa  mkoa  wa  Iringa  na  wafanyakazi  wote   kujitokeza kwa wingi  kumlaki Rais  wetu mpendwa  wetu Dkt  John  Magufuli .
Mkuu  wa mkoa wa  Iringa  Amina  Juma Masenza


Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya katikati akiongoza kuimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa kikao na  wanahabari mjini  Iringa .
..................................................................................................................................................

No comments:

Post a Comment