Balozi Mdogo wa Oman Visiwani Zanzibar, Ahmad
Mohamed Al Muzaini wa nne kutoka kulia akiwa amesimama baada ya
kumaliza kuzungumza kwenye maonyesho ya makazi ya Oman Visiwani Zanzibar
yakiandaliwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman.
Maonyesho hayo yamefanyika katika Hoteli ya The Park Hyatt, Zanzibar.
Wengine ni wadau wa ardhi na makazi waliohudhuria kwenye maonyesho hayo.
Picha na Mpiga picha wetu.
Na Mwandishi
Wetu, Zanzibar
HUKU
maonyesho ya makazi ya Jebel Sifah yanayoonyeshwa na Kampuni ya Muriya yenye
maskani yake nchini Oman yakiendelea visiwani Zanzibar katika Hotel ya The Park
Hyatt, baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, wafanyabiashara wa visiwani
hapa wametakiwa kupanua wigo wao wa kibiashara kwa kununua makazi yao nchini
Oman ili wajiwekee vitega uchumi kwa ajili ya maendeleo yao.
Ushauri huo
umetolewa leo na Meneja Mauzo wa Muriya, Ghizlane El Gouchi, wakati wa
kuelimisha wakazi na wananchi wa Zanzibar juu ya utendaji kazi wao katika sekta
ya ardhi na makazi waliyojikita nchini Oman, huku wakijivunia maendeleo makubwa
kwenye sekta hiyo muhimu dunian kote.
Wadau wa ardhi na makazi nchini Tanzania, Ali Al Maskary kulia na Aflah Al Maskary kushoto wakifuatilia jambo na mdau wa ardhi kutoka Oman, Faisal Said Rashid Alzakwani katika maonyesho ya makazi yanayoendeshwa na kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman kwa ajili ya kununua makazi nchini humo. Tukio hilo linafanyika leo Aprili 6, katika Hoteli ya The Park Hyatt, Zanzibar kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni.
Faisal Said Rashid Alzakwani kushoto akipiga picha na aalozi mdogo wa Oman Visiwani Zanzibar, Ahmad
Mohamed Al Muzaini.
Alisema
kwamba ni vyema Watanzania wote wakiwamo wafanyabiashara wakaelewa umuhimu wa
kujitanua kibiashara kwa kuangalia uanIshwaji wa biashara nje ya mipaka yao,
huku Kampuni yao ikifungua milango kwa kuwauzia makazi kwa utaratibu mzuri na
rahisi katika maeneo yenye solo kama vile pembeni mwa bahari ambako wanaweza
kuyatumia kama fursa za kiuchumi bila kusahau hati ya kuishi nchini Oman.
Muriya ni
kampuni kubwa iliyojikita katika utoaji wa huduma za makazi na utalii nchini
Oman, ambao kwa wiki moja sasa wanaendelea na maonyesho yao ya kibiashara
wakianzia jijini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar kama njia ya kubadilishana
mawazo na kuwajulisha Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla juu ya biashara zao.
“Umuhimu wa
biashara ni kupanuka kutoka eneo dogo kwenda eneo kubwa, hivyo ni lazima wadau
wa Zanzibar kutafuta fursa nyingine hususan za kuwekeza nchini Oman katika eneo
la makazi ambayo tutawauzia na wao watalipa kwa awamu ndani ya kipindi cha
miaka miwili, tukiamini kuwa kwa wale wenye malengo wanaweza kufanikiwa, ambapo
asilimia 10 zitalipwa baada ya kujisajili, huku gharama zetu zikianzia Dola
98,000 tu,"Alisema.
Kwa mujibu
wa El Gouchi, mradi wao wa Jebel Sifah ni mwendo wa dakika 40 tu kutoka Muscat,
karibu na ufukweni ambayo yana ukubwa hadi wa square meter 365,000, ukiwa ni
mradi mkubwa unaowahusu Watanzania wote na ni fursa nzuri za uwekezaji.
Maonyesho
hayo ya kibiashara ya makazi yanayouzwa na Kampuni ya Muriya, yamefanyika
jijini Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa tangu Aprili 3 hadi 5, ambapo kwa
wakazi wa Zanzibar wenyewe wamefanikiwa kufikiwa na maonyesho hayo jana Aprili
6 katika Hoteli ya The Park Hyatt kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wananchi
wanakuwa na elimu juu ya umuhimu wa uwekezaji kwenye sekta ya makazi.
No comments:
Post a Comment