Na Ripota wetu Kasulu, Kigoma
MAAMBUKIZI
ya viashiria vya ugonjwa wa Malaria Nchini Tanzania yame pungua kwa
Watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 na kufikia
asilimia 7.3 kwa Mwaka 2017 hii ni kuzigatia harakati zinazo fanywa na
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mashirika ya Marekani (USAID) pamoja
na shirika la WHO kuhakikisha wanautokomeza ugonjwa huo.
Akizindua
takwimu zilizo tolewa na Ofisi ya Takwimu ya Tanzania leo Wilayani
Kasulu Mkoani Kigoma Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na
watoto Ummy Mwalimu , alisema Siku ya leo kupitia maadhimisho hayo
yaliyofanyika kitaifa Kigoma, atazindua rasmi Matokeo ya Utafiti wa
Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017.
Kwa
Mujibu wa Mkurugenzi mkuu ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Albina Chuwa
alithibitisha Matokeo ya sasa ya utafiti huu, yanaonesha kuwa kiwango
cha malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini
Tanzania kimeshuka kwa Zaidi ya nusu kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015
hadi asilimia 7.3. Hii ni kwa kutumia kipimo cha haraka cha utambuzi wa
vimelea (mRDT).
Waziri
Ummy alisema utafiti huo unaonesha Mikoa yenye kiwango kikubwa cha
watoto wenye malaria ni, Kigoma (asilimia 24.4), Geita (asilimia 17.3),
Kagera (asilimia 15.4) na Tabora (asilimia 14.8) ambapo Mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro, Manyara, Njombe, Songwe na Dodoma ina kiwango kidogo cha
maambukizi chini ya asilimia moja.
"Takwimu
hizi, zinaonesha kupungua kwa kiwango cha malaria kwa kiasi kikubwa, na
hii ni habari njema kwetu sote na inaonesha ni jinsi gani Serikali yenu
ipo tayari kutoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa malaria
inadhibitiwa na hatimae tuweze kuitokomezwa kabisa Ili kuhakikisha lengo
hilo linafanikiwa, tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja katika kufikia
malengo tuliyojiwekea ili jamii, hasa watoto chini ya umri wa miaka
mitano na wanawake wajawazito ambao ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa
wa malaria waweze kuepukana na ugonjwa huu", alisema Waziri Mwalimu.
Alisema Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, lakini bado kuna
changamoto, ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili kwa pamoja tuweze
kufikia malengo ya kutokomeza malaria nchini.
Changamoto
hizo ni pamoja na Wanajamii kutotumia vyandarua ipasavyo katika
kujikinga na ugonjwa wa malaria, kuwepo kwa mitazamo potofu juu afua za
kupambana na malaria; mfano dhana ya kuwa viuatilifu-ukoko za
kunyunyizia ukutani zinaleta kunguni na viroboto na kuwa vyandarua
vinapunguza nguvu za kiume ni dhana potofu ambazo hazina ukweli wowote.
Vilevile, Jamii kutoshiriki kikamilifu katika kutunza mazingira na
kuharibu mazaliaya Mbu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mwakilishi wa shirika la misaada na Maendeleo la
Marekani USAID Andy Karas alisema kwa zaidi ya miaka 12 USAID imekuwa
ikifanya kazi pamoja na serikali kupitia Wizara ya Afya kwaajili ya
Kupambana na Malaria.
Alisema
watoto wengi walio hai leo ni kwa juhudi za serikali, kwa kushirikiana
na Mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria kwa Muda wote
wameweza kusambaza vyandarua zaidi ya milioni 10 na kununua viuwadudu
zaidi ya milioni 20 na kupuliza dawa ya Mbu kwenye maeneo hatarishi vile
vile wameweza kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kufanya
takwimu mbalimbali juu ya kupungua kwa ugonjwa wa Malaria.
Nae
Balozi wa Usizwi Florence Tinguell aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya kwa juhudi kubwa walizo zifanya katika
kuhakikisha wanatokomeza Malaria ,imeweza kubuni mbinu. Kwa zaidi ya
miaka 50 Ubalozi wa Uswizi umekuwa ukifadhili tafiti za malaria ambazo
zimekuwa zikifanywa na taasisi ya Ifakara Health Institute.
Hata
hivyo mjumbe wa kamati ya bunge ya kupambana na Malaria ( TAPAMA) na
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa Rose Tweve alisema wao kama
wabunge wanatoa wito kwa Wananchi wote kuwa jukumu la kupambana na
Malaria na mapambano dhidi ya Malaria ni la Wananchi na wasiiachie
serikali peke yake na kuomba nguvu kubwa ielekezwe kwenye kinga na
wahudumu wa Afya na wakina mama kufika hospitali kwa wakati ilikuweza
kupatiwa kinga ya Malaria.
Kilele
cha Maadhmisho ya Malaria kimefikia tamati leo kwa kufanyika katika
wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO
TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
Waziri
wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu
akionyesha rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka
2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya
malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni Waziri wa
Elimu Joyce Ndalichako – kwanza kulia, Balozi wa Uswizi ha Tanzania
Florence Tinguell na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima
Maulid na Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu
akimkabidhi Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako Matokeo ya Utafiti wa
Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua
wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu
Mkoani Kigoma. Wengine ni– kwanza kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Afya Zanzibar Halima Maulid na na Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania
Andy Karas.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu
akimkabidhi Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.Matokeo ya
Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya
kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika
Kasulu Mkoani Kigoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Takwimu
Tanzania – NBS Albina Chuwa.
Picha
ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa Serikali na
viongozi wa mashirika mbali mbali ya kimataifa, wakiwa katika viwanja
vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya
Malaria duniani.
Waziri
Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
kushoto akipokea ramani ya Tanzania inayoonyesha maeneo yaliyopungua kwa
malaria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.
Albina Chuwa wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Malaria Duniani
Mkoani Kigoma,pichani kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania
Andy Karas.
Afisa
Mradi JOHNS HOPKINS VectorWorks Jacqueline Madundo akitoa maelezo
mafupi kuhusu mfumo unaosimia uwajibikaji katika maswala ya vyandarua
nchini kwa Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa kilele
cha Maadhmisho ya Malaria yaliyofanyika leo katika wilaya ya Kasulu
Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA
MALARIA WEWE JE?
Kundi
la muziki wa Bongo fleva la WEUSI wakiwa jukwaani kutoa Burudani na
Elimu juu ya kinga ya ugonjwa wa Malaria ambayo imehadhimishwa katika
viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya
siku ya Malaria duniani.
Kundi
la wananchi lililojitokeza katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu
mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ili
kusikiliza ujumbe kuhusu Malaria, mgeni rasmi wa tukio hilo ni Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
(MB).
No comments:
Post a Comment