Mwenyekiti
wa CCM Mkoa Bi. Kate Kamba ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya
Kigamboni kwa utekelezaji wa Ilani wa chama cha Mapinduzi na kusema kuwa
ameiona thamani ya fedha katika miradi yote aliyoitembelea hivyo
mshikamano uliopo uendelezwe.
Amayezungumza
hayo jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi aliyoifanya
Manispaaa ya Kigamboni yenye lengo la kuona ni naman gani Ilani ya Chama
inatekelezwa.
Akizungumza
na watumishi na wananchi wanao shiriki kusimamia miradi Bi.Kamba
amesema kuwa, Miradi yote inatekelezwa katika ubora na ndani ya wakati
na thamani ya fedha ( Value for money) inaonekana.
"Miradi
yenu mizuri na inatekelezwa kwa ubora na wakati, mnaspidi nzuri sana
hii inaonesha ni naman gani mnaushirikiano, Kigamboni ni Wilaya changa
lakini mambo mnayofanya mnawazidi hata Wilaya kongwe, tumependa" Alisema
Kamba
Aliongeza
kuwa ameona ushirikishwaji katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba
jamii imeshiriki kikamilifu hali inayopelekea kuona wanao wajibu wa
kutunza na kusimamia miradi yao ndio maana wameweza hata kufikia
makubaliano ya kuomba punguzo la bei ya ununuzi wa vifaa vinayohitajika
kwenye ujenzi miradi.
Aidha
Bi. Kamba alisema kuwa sheria ya manunuzi inagharimu sana utekelezaji
wa miradi , urasimu mwingi tofauti na utaratibu wa local fundi
unaosaidia kutumia fedha kidogo na miradi kujengwa kwa wakati huku
thamani ya fedha ikionekana. Kamba aliwataka watumishi kuona anao wajibu
na sehemu yake ya kufanya kazi na kuhudumia wnanchi ikiwa ni
utekelezaji wa ilanai na kuhakikisha lengo lililowekwa linafikiwa kwa
kiwango cha juu.
Kwa
upande wake a Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa alisema
kwamba yeye pamoja na Madiwani , Mkurugenzi na watendaji wake wanaimba
wimbo mmoja , thamani ya fedha inayoonekana katika kila mradi ni matokeo
ya usimamizi uliopo ambao wamepewa na mamalaka kusimamaia.
Ameongeza
kuwa kigamboni inaweza kuwa ya kwanza kwa Halmashauri zinazotekeleza
ujenzi wa makao makuu tangu kuanzishwa kwani ndani ya kipindi kifupi cha
miaka 2 tangu kuanzishwa kwake na watumishi watakuwa tayari kwenye
jengo lao la Utawala lenye ghorofa 3, hii imewezekana kutokana na mfumo
mzuri wa matumizi ya fedha.
Aidha
alisema kuwa mfumo unaotumika wa mafundi wenyeji unaokoa kiwango
kikubwa cha fedha ambazo zilikuwa zinapotea bila sababu katika mfumo wa
manunuzi.
"Nadhani
tuendelee kuangali hizi sheria za manunuzi, zinazumiza sana Serikali na
tuanze kufuata taratibu za kawaida, mfano mfuko wa misumari kwa mfumo
wa manunuzi unaweza nunua hadi elfu 6000, wakati kawaida unanunua
elfu3000 hadi elfu 3500"Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephene Katemba alisema kuwa anashukuru
kutembelewa na viongozi wake na kuona namna gani Ilani ya Chama inatekelezwa,
Amesema
hadi sasa ameshapokea Bilion 2 kwaajili ya ujenzi wa jengo la utawala
na taratibu zote zimezingatiwa za kupata mkandarasi , mradi unayobond ya
kulinda( secured bond) na performance bond ( fedha zitekelezwe kwa
kadri inavyotakiwa).
Mwisho
alishukuru ujio wa viongozi wa Chama na kwamba kwake ni hamasa kubwa
hivyo yeye kama kiongozi atajitahidi kuhakikisha miradi yote
inatekelezwa kwa kadri ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotaka.
Ziara
ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa iliyoambatana na viongozi mbalimbali wa Chama
walipata fursa ya kutembelea mradi wa ukarabati wa Zahanati ya Buyuni,
Ujenzi wa kituo cha Afya Kimbiji, Ujenzi wa miundombinu ya Shule
kwaajili ya kuanzisha kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari Nguva,
ujenzi wa jengo la utawala na ujenzi wa uanzishwaji Sekondari eneo la
Shule ya Msingi Kigamboni.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bi. Kate Kamba akizungumza na kutoa pongezi zake kwa Manispaa ya Kigamboni.
Baadhi ya Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa alipokuwa akizungumza nao
jengo la wamama wajawazito likiwa kwenye hatua ya renta
Jengo la maabara na upasuaji likiwa katika hatua ya upauaji kama inayoonekana katika picha
muonekano wa jengo la kuhifadhia maiti
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni akiwa ameongozana na viongozi nyingine kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kimbiji.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigamboni Dk.Charles Mkombachepa akitoa maelekezo ndani ya jengo la maabara na upasuaji
No comments:
Post a Comment