Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
HALMASHAURI
182 nchini ikiwemo saba za mkoani Pwani ,zinadaiwa kutumia vibaya
mabilioni ya fedha yaliyotumika kuondoa zaidi ya lita 100,000 za dawa ya
viuadudu vya mazalia ya mbu ,zilizokosa soko katika kiwanda cha Biotech
Products Limited,kilichopo Mji Wa Kibaha ,ikiwa ni agizo alilolitoa
Rais Dkt.John Magufuli June 22 mwaka jana.
Aidha
halmashauri ambazo zinadaiwa kiasi cha sh.bil.1.8 walizochukulia dawa
hiyo zimetakiwa kulipa fedha hiyo haraka ili kiwanda kiweze kujiendesha
na kulipa watumishi wake mishahara.
Akizungumza
katika ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa ya
viuadudu inayozalishwa katika kiwanda hicho ,meneja wa udhibiti wa ubora
na viwango kiwandani hapo , Samwel Mziray , alisema ni halmashauri
mbili pekee zilizochukua dawa hiyo kwa awamu ya pili.
Alieleza
halmashauri 184 zilichukua dawa kwa awamu ya kwanza na ya pili zaidi ya
lita 200,000 ambazo wameziweka stoo bila kuzitumia wakidai hawana fedha
ya kununulia pampu."Wanashindwa kuzitumia kutokana na kukosa pampu ya
kupulizia ,hii ni aibu ,nimesikitishwa sana na hali hii, "
"Ni
ngumu na jambo la ajabu leo hii Rais atoke kuja kufuatilia agizo lake
ama kuzifuatilia halmashauri hizo, serikali ina nia njema lakini
watendaji tunashusha juhudi za Rais na serikali ""Ninawaomba wakuu wa
mikoa mingine nchini kuiga mfano wa mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi
Evarist Ndikilo ya kuhamasisha kununua dawa hizo, ili kupambana na vita
dhidi ya ugonjwa hatari wa malaria." alieleza Mziray .
Mziray
alieleza baada ya agizo la Rais walianza na mikoa 14 katika halmashauri
96 na awamu ya pili waligawa kwenye halmashauri za mikoa 12 na kutimiza
mikoa 26 na halmashauri 184 nchini .Hata hivyo baada ya mgao wa kwanza
halmashauri ya Rufiji iliongeza Lita 540 na Kibaha Vijijini waliongeza
lita 520 .
Mziray
alifafanua nchi ya Niger wameshawaunga mkono Kwa kununua dawa hiyo
pamoja na Angola ambayo imeagiza lita 106,020 lakini cha kustaajabisha
Tanzania na Kibaha Mjini bado hawajatambua umuhimu huo.Aliwataka
wakurugenzi wa halmashauri na jamii kujitokeza kununua dawa ya viuadudu
ili kuondokana na vifo vinavyotokana na malaria.
Nae
mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alikitaka kiwanda hicho
kijitangaze katika vyombo mbalimbali vya habari na kutoa elimu kwa
jamii kuwa madawa hayo hayana madhara kwa matumizi ya binadamu .Alisema
biashara bila matangazo haijiuzi hivyo ni wakati wa kujitangaza ili hali
kuinua soko na kutambulika.
Pia
Ndikilo alieleza halmashauri zilizofungia dawa hizo ni aibu "sijui
tumelongwa nini,malaria ipo dawa ipo hatununui ,hivi tunasubiri Rais aje
tena atununulie tena dawa ,haiwezekani"
"Nchi
imetumia dollar milioni 22 ,wafanyakazi 127 wanakosa mishahara yao pale
kiwandani,leo halmashauri hazioni hili ????ni lazima watumie dawa hizi
na kupata matokeo" alisisitiza Ndikilo.
Mkuu
huyo wa mkoa alikemea tabia hiyo na kuwataka wachukue dawa na kuchukua
nyingine pasipo kufungia stoo na kudai atakaerudia makosa aondoke kwenye
nafasi yake mara moja.Ndikilo
alisema hatomvumilia mkurugenzi anachezea mamilioni ya fedha
wanayotenga kwa ajili ya kupambana na malaria ,na atakaejiona hatoshi
aanze kuondoka katika nayadhifa yake kupisha wengine.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, Yudas Ndungile ,alisema idara
ya afya mkoa inahimiza matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu
vya muda mrefu.
Alibainisha
,mwaka 2017 vyandarua 59,494 viligawiwa mashuleni pia vyandarua 48,120
viligawiwa kwenye kliniki na mwaka 2016 vyandarua 877,297 viligawiwa
katika ngazi ya kaya na familia .
Ndungile
alielezea wanakabiliana na malaria na kutoa elimu ya usafishaji wa
mazingira kwa kuondoa mazalia ya mbu kwenye madimbwi ,suala lililosaidia
vifo vinavyotokana na malaria kupungua na malaria kushuka kuwa ugonjwa
wa pili kati ya magonjwa yanayoongoza kimkoa.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jennifer Omolo alisema wameitikia wito
uliotolewa na mkuu wa mkoa na wanakwenda kuagiza lita 720 ili kuua
mazalia ya mbu wa malaria.
Omolo alisema kuwa awali walichukua lita 520 ambazo walizitumia ,na wanaahidi kutoweka stoo .
Mkuu
wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo (wa kulia) ,akimkabidhi dawa
ya viuadudu vya mazalia ya mbu ,mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze
,Edes Lukoa wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa
dawa hiyo ,Mkoani Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Meneja wa
udhibiti wa ubora na viwango katika kiwanda kinachozalisha dawa ya
viuadudu cha Tanzania Biotech Products Ltd kilichopo Mjini Kibaha
akionyesha wananchi kuwa dawa hiyo haina madhara, wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa hiyo,Mkoani Pwani .(picha na Mwamvua Mwinyi)
No comments:
Post a Comment