Thursday, April 12, 2018

DC ILALA AWATAKA WAJASIRIAMALI WANAWAKE KUJIUNGA NA JUKWAA LA WANAWAKE



Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kikundi cha Wajasiriamali cha Mshikamano Mchikichini Sokoni katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Katibu wa Kikundi hicho, Juliana Richard, Mwenyekiti, Anjela Mwamakula na aliyevaa miwani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita.
Wanachama wa Kikundi cha Mshikamano Mchikichini Sokoni wakiwa kwenye uzinduzi wa kikundi chao.
Hapa wakiserebuka.
Mwenyekiti wa Soko la Mchikichini-Ilala Jumanne Kongogo akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Wakiimba na kucheza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Anjela Mwamakula akisoma taarifa ya kikundi mbele ya mgeni rasmi.
Makofi yakipigwa.
Umakini katika uzinduzi huo.
Katibu wa Kikundi, Juliana Richard akimkabidhi mgeni rasmi risala yao.
Mkurugenzi wa Shirika la EfG, Jane Magigita akizungumza katika uzinduzi huo.
Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akihutubia wakati akizindua kikundi hicho.
Mkurugenzi wa Shirika la EfG, Jane Magigita akionesha cheti cha kikundi hicho baada ya kuzinduliwa.
Mwenyekiti wa kikundi hicho, Anjela Mwamakula na Katibu wake Juliana Richard (kulia), wakionesha cheti.
Mwakilishi wa Ofisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Ilala, Regina Ng'ongolo, akizungumza.
Ofisa Ushirika Manispaa ya Ilala, Donald Kibhuti akizungumza machache kwenye uzinduzi huo.
Ofisa kutoka ofisi ya Sheria na Msajili Msaidizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Geofrey Mlagala, akizungumza.
Mlezi wa Kikundi hicho, Betty Mtewele akizungumza.
Zawadi zikitolewa kwa mgeni rasmi.
Mjasiriamali Godliver Massawe (kulia), akimuonesha mgeni rasmi bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanawake hao.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi


Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE Wajasiriamali wametakiwa kujiunga na Jukwaa la Wanawake ili kujiinua kiuchumi.

Mwito huo umetolewa na Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakati akizindua kikundi cha wajasiriamali cha Mshikamano Mchikichini Sokoni katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana.

Katika hatua nyingine Kalekezi amewataka wanawake hao kuacha unafiki na kupendana jambo litakalowasaidia kusonga mbele kwenye umoja wao huo.

Alisema Dunia imeanzisha Jukwaa la Wanawake ambapo wanawake watakuwa wakukutana kujadili changamoto walizo nazo na jinsi ya kuzikabili pamoja na kuangalia fursa mbalimbali za maendeleo."Jukwaa ili na sisi linatuhusu hivyo hatuna budi kujiunga nalo kwani huko tutapata wataalamu waliobobea katika masuala mbalimbali pamoja na biashara hivyo ni vizuri tukalichangamkia" alisema Kalekezi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality fo Growth (EfG) Jane Magigita alisema wakati huu si wakulala bali ni wakuangalia fursa nyingine ili kujikomboa kiuchumi.Alisema Serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kupambana vilivyo ili kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi.

Mkurugenzi huyo ambaye kupitia shirika analoliongoza la EfG amekuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa wanawake alisema hivi sasa kwa Dar es Salaam semina zimekwisha badala yake wanakwenda katika mikoa nane ambapo wataanzisha kampeni ya uhamasishaji kupinga ukatili wa kijinsia masokoni ambapo wasaidizi wa kisheria waliopata mafunzo kutoka shirika hilo ndio watakao kuwa wahamasishaji wakubwa.

"Sasa hatutakuwa tena na semina tunakwenda kufanya uhamasishaji mkubwa mkoani tutakuwa na basi letu maalumu katika kampeni hiyo" alisema Magigita.

Katibu wa kikundi hicho, Juliana Richard wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi alisema changamoto yao kubwa ni miundombinu mibovu katika soko lao la mchikichini na mikopo wanayokopa kuwa na riba kubwa.Alisema kikundi hicho kwa sasa kinamtaji wa sh.milioni 11 lakini lengo lao kwa kiasi cha chini kuwa na sh.milioni 70.

Ofisa kutoka ofisi ya Sheria na Msajili Msaidizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Geofrey Mlagala alisema wanawake ambao wapo tayari kuanzisha vikundi vyao milango ipo wazi na watasaidiwa kuelekezwa namna ya kuvifungua.

No comments:

Post a Comment