Monday, March 5, 2018

MNEC SALIM ASAS ATOA MILIONI 24 KWA AJILI YA MAENDELEO YA UWT WILAYA YA MUFINDI

Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi. Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akikabidhiwa shati na umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Mufindi baada ya kukabidhiwa kofia ambayo ameifaa hapo 
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akifurahia jambo na viongozi wa chama hicho pamoja na wabunge wa viti maalum mkoa wa Iringa.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi.

Pesa hizo zimetolewa wakati wa baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Mufindi mkoani (UWT) lilofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo mjini Mafinga na kuhudhuriwa na wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati,Rose Tweve na mama Mwamwindi.

Akizungumza katika baraza hilo MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa wilaya ya mufindi kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.

Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema Asas 

Asas alisema kuwa nimesikia mnataka kujenga kipanda kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja huu,hilo ni jambo bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha shilingi milioni sita ili mfikie malengo yenu.

“Sijaona changamoto ila nimeona matarajio ambayo ni kuanzisha mradi wa kuuza sare za chama,kumalizia ujenzi wa vibanda vya umoja wenu,kutafuta eneo la ekar 5 kwa ajili ya kilimo cha viazi na kupanda miche ya miparachichi na kutafuta kiwanja kikubwa kwa ajili ya uwekezaji na ndio sababu iliyonifanya niwachangie kiasi hicho cha pesa” alisema Asas

Aidha Asas alimpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kwenye kata kumi na saba kwa kutoa kiasi cha silingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC alisema kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata kwa kata zote 36 za wilaya ya Mufindi.

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Mufindi Mwanaidi Kaleghela alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa milioni ishirini na nne kwa UWT mufindi.

“Ametoa shilingi mioni sita kwa UWT na ametoa milioni kumi na nane kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kaleghela

No comments:

Post a Comment