Wednesday, March 21, 2018

DRAW YA PLAY-OFF YA CAF CONFEDERATION CUP

-Draw ya mechi za Play-Off za Caf Confederation Cup kufanyika leo makao makuu ya CAF, Cairo Misri majira ya Saa 8:30 Mchana

-Draw hiyo inahusisha timu 32 timu 16 ambazo zilitolewa kwenye klabu bingwa Afrika (Caf Champions Leagu) na timu 16 ambazo zilifuzu hatua ya 16 bora kutoka kombe la Shirikisho (Caf Confederation Cup)

-Kutakuwa na Pot 4, ya Kwanza ni Pot A itakuwa na timu 4 ambazo zipo juu kwenye Rank ya klabu  kwa timu zilizotolewa kwenye Caf Champions League timu hizo ni Al hilal Omdurman (Sudan), St George (Ethiopia), As Vita Club (DR Congo) na Zanaco (Zambia).

-Pot ya Pili ni Pot B ambayo itakuwa na timu 4 ambazo zina Rank kubwa kwa vilabu kutoka kwenye timu 16 ambazo zilifuzu 16 bora ya Caf Confederation Cup timu hizo ni USM  Alger (Algeria), Super Sport United (Afrika kusini), Hilal Obayed (Sudan) na Enyimba (Nigeria).

-Pot ya Tatu ni Pot C ambayo itakuwa na vilabu 12 ambavyo vimebaki zilizotolewa kwenye Caf Champions League Timu hizo ni UD Songo (Msumbiji), Yanga Sc (Tanzania), CF Mounana (Gabon), Bidvest Wits (Afrika Kusini), Williamsville AC (Ivory Coast), Génération Foot (Senegal), Mountain On Fire (Nigeria), Plateau United (Nigeria), Gor Mahia (Kenya), Asec Mimosas (Ivory Coast), Rayon Sports (Rwanda) na Aduana Stars (Ghana).


-Na Pot ya 4 itakuwa Pot D ambayo itakuwa timu 12 ambazo zimebaki baada ya kutoa 4 (16-4=12) ambazo zilifuzu kutoka Caf Confederation Cup timu hizo ni La Mancha (Congo Brazzavile), Belouizdad  (Algeria), Djoliba (Mali), RSB Berkane (Morroco), Raja Casablanca (Morocco), Al Masry (Misri), Fosa Juniors (Madagascar), CARA Brazzavile (Congo Brazzaville), Costa do Sol (Msumbiji), Akwa United (Nigeria), Deportivo Niefang (Equatorial Guinea) na Welayta Dicha (Ethiopia)


-Wataanza draw na Pot A  vs Pot C kwa timu 4 kutoka Pot A na Timu 4 kutoka Pot C. wanaenda Pot B vs Pot D kwa timu 4 kutoka Pot B na Timu 4 kutoka Pot D baada ya hapo zitakuwa zimebaki timu 8 kutoka Pot C na Timu 8 kutoka Pot D wanachezesha tena Pot C vs Pot D kwa timu 8 kutoka Pot C na Timu 8 kutoka Pot D hapa maana yake ni kwamba timu ambazo zipo Pot A na Pot B haziwezi kukutana  kutokana na kuwa na ranking kubwa Afrika kwa miaka 5 iliyopita.

NB:- Rank ninayozungumzia hapo Pot A na Pot B ni rank ya Performance ya klabu yenyewe sio nchi.


-Baada ya Draw mechi za Play Off zile za mkondo wa kwanza kuchezwa april 6-8 na zile za marudiano kuchezwa April 17-18 bàada ya hapo April 21 itachezeshwa Draw tena ya makundi manne kwa timu 16 zilitakazofuzu Makundi ya Caf Confederation Cup


DRAW YA MAKUNDI YA CAF CHAMPIONS LEAGUE .


-Pia kutafanyika draw ya makundi ya Caf Champions League. Timu 16 zilizofuzu hatua ya makundi zimepangwa kwenye Pot 4 kulingana na kiwango (rank) cha timu kwa miaka mitano


-Pot 1 wapo Tp Mazembe (DR Congo), Al Ahly ( Misri), Etoile deu Saleh (Tunisia) na Wydad Casablanca (Morocco)


-Pot 2 wapo Mamelodi Sundowns (Africa Kusini), Esperance de Tunis (Tunisia) Zesco United (Zambia) na Entente Setif (Algeria)


-Pot 3 zipo Mc Alger (Algeria) KCCA (Uganda) Horoya (Guinea) na Mbambane Swallows (Swizland)


-Pot 4 wapo 1° de Agosto, Townships Rollers (Botswana), Difaa El Jadidi (Morroco) na As Togo Port (Togo)


Mechi za Hatua ya makundi ya Caf Champions League kuchezwa

-Mechi za kwanza zitachezwa may 4-6

-Mechi za pili zutachezwa may 15-16

-Mechi za tatu zitachezwa July 17-18

-Mechi za nne Zitachezwa July 27-29

-Mechi za tano zitachezwa August 17-19

-Mechi za sita zitachezwa August 28-29


-Mechi za makundi ya Caf Champions League zitakuwa zimeisha Draw ya Robo fainali itapangwa September 03, 2018 Cairo Misri tena na mechi za Robo fainali, nusu fainali na fainali ni mtoano na zitakuwa hivi

-Robo fainali mechi za mkondo wa kwanza kuchezwa September 14-16 na zile za marudiano kuchezwa september 21-23

-Nusu fainali ya Caf Champions League kuchezwa October 2-3 kwa michezo ya mkondo wa kwanza wakati mechi za mkondo wa pili kuchezwa October 23-24

-Fainali kuchezwa November 2-4 kwa mechi ya mkondo wa kwanza na wakati mechi ya marudiano ni November 9-11

No comments:

Post a Comment