Sunday, February 4, 2018

WANANCHI BOMBABILI WAPEWA SOMO UPIMAJI WA ARDHI

Na David John

WANANCHI wa mtaa wa Bombambili Kata ya Kivule wamepewa somo kuhusu suala zima la upimaji wa ardhi, huku wakielezwa umuhimu wa kurasimisha ardhi yao kwa lengo la kuzifikia huduma mbalimbali za kiserikali

Akizungumza katika mkutano wa wananchi wa mtaa huo ambao uliitishwa na ofisi ya Serikali hiyo. Adolph Milunga ambaye ni mtalaamu mpimaji kutoka chuo cha ardhi mkoani Morogoro aliwaeleza wananchi hao umuhimu wa kupima ardhi na faida Zake.

Amesema hata kuchagua watalaamu kutoka chuo cha Ardhi Morogoro hawajafanya Makosa Kwani ni uhakika kwamba serikali ndio inasimamia ambapo kupimwa kwa ardhi kunakufanya kuondoka kwenye umasikini.

Ameongeza kuwa kupimwa kwa ardhi kunakuwezesha kupata dhamana Mahakamani na mambo mengine kama mirathi. Lakini pia mikopo kwa urahisi tofauti na kuwa na ardhi ambayo haijapimwa.

" wao kama watalaamu wa serikali wanafanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa mno na kwenye mtaa huu tumetoa ofa ya 160,000 na ofa hii itadumu kwa wiki moja. "alisema . Pia amesema baada ya kumalizika kwa wiki moja hakutakuwa tena kwa maana ahadi tena ya ofa hata hivyo watakwenda kuchungulia na kuona kuna nini kipo huko Benki.

"kuhusu hati baada ya mchakato wa upimaji kumalizika zitakuja kukabidhiwa katika mtaa huo tena ikiongozwa na Waziri husika wa ardhi. Nakusisitiza kuwa watakuwa tayari kwenda nawale ambao wako Tayari kufanya nao kazi. "amesema Milunga.

Hata hivyo Mwenyekiti wa mtaa huo. Moses Malela aliomba watalaam had wa upimaji kuongeza ofa hiyo angalau iwe ya wiki mbili . Kwaupande mwingine Mtalaamu huyo alikubaliana na Mwenyekiti huyo wa serikali nakusisitiza kwamba atatoa majibu halisi ijumaa ya wiki inayoaza kesho.

Pia mtalamu huyo alitoa ofa nyingine kwa taasisi za dini kwa kuchangia shilingi 100000 ili nao waweze kupimiwa huku akitangaza ofa nyingine kwa watu wasiojiweza kabisa. Wakati huohuo mwenyekiti aliwahamasisha wananchi wake kupima ardhi nakusisitiza kwamba faida hiyo sio ya serikali bali ni ya kwao.

Amesema kupima ardhi nikufungua vichocheo vya maendeleo ikiwa pamoja na kukaa katika maeneo ambayo yamepimwa na hayo pia ilikuwa nimoja ya ahadi zao wao kama viongozi kwamba watahakikisha wakiingia watapambana ili kuona ardhi yao inapimwa.

Selemani Kimeya alishukuru mchakato huo wa upimaji lakini alidai kiwango cha pesa iliyotajwa kulipa kwa mara moja ningumu nakuhoji kwanini wasilipe mara mbili. Salimin Issa naye alisema hadi wanakwenda kwenye mkutano kero kubwa ilikuwa ni shilingi 310,000/= hawana na hiyo pesa badala yake wangepunguza zaidi.

Aidha wananchi hao pamoja na mambo mengine lakini walikuwa wanahitaji kamati yao ili iweze kusimamia mchakato huo nakudai kamati hiyo iliyokuwepo ni ya zamani ambayo ilikuwa kivule na sasa bombambili hata hivyo walifafanuliwa juu ya hilo na mwisho kukubaliana na kamati iliyopo. 

No comments:

Post a Comment