Monday, February 26, 2018

PLAN INTERNATIONAL,UMOJA WA ULAYA YAWAWEZESHA KIUCHUMI VIJANA 592 WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU KIBAHA

Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tamisemi Sememani Jafo Kulia wa Meneja wa mradi wa Yee kutoka Shirika lisolokuwa la kiserikali la Plan international Simon Ndembeche wa kushoto wakikagua vifaa mbavyo vimetolewa kwa vijana wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kiluvya Wilayani Kisrawe katika halfa fupi ya kukabishi vitendea kazi
Diwani wa kata ya Kiluvya Aidan Kitare akizungumza jambo wakati wa sherehe ya kukabiddhi vifaa kwa vijana wa kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe ambao wanaishi katika mazingira magumu, ambapo wamesomeshwa na kupatiwa vitendea kazi na shirika la Plan International kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na janga la umasikini.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akizungumza katika halfa ya kukabidhi vifaa kwa vijana wa kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe ambao wanaishi katika mazingira magumu, na wengine yatima.
Baadhi ya vijana wanaoishi katika mazingiza magumu katika kata ya Kiluvya Wilayani Kibaha ambao wamewezeshwa kiuchumi na shirika la Plan Innternationala ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasisiki.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU


VICTOR MASANGU, KISARAWE

JUMLA ya vijana wapatao 592 wanaoishi katika mazingira magumu,yatima,na wasichana waliopata mimba katika umri mdogo kutoka katika Wilaya ya Kisarawe Kibaha Mkoani Pwani wamewezeshwa kwa kupatiwa mafunzo ya ufundi stadi wa aina mbali mbali pamoja na kukabidhiwa vifaa vya kazi kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini ambalo limekuwa likiwakabili.

Vijana hao wamepatiwa msaada wa vifaa mbali mbali vya kuendeshea shughuli za ujarisiamali kupitia mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi ujulikanao kwa jina (YEE) ambao unasimamiwa na Shilika lisilokuwa la kiserikali la Plan Internationala kwa ufadhili wa jumuiya ya umoja wa Ulaya.

Wakizungumza katika halfa fupi ya makabidhiano hayo baadhi ya vijana hao walionufaika na mradi huo akiwemo Magnalena Mwendo na Piusi Charles walisema kwamba msaada huo na mafunzo na vifaa walivyopatiwa vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini ambapo pia wameiomba serikali kuwasaidia kupata mikopo ya fedha mfumo wa maendeleo ya vijana.

“Sisi vijana tumefarijika sana kwa kupata vifaa hivi ambavyo kwa kweli vitaweza kutusaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondoka na janga la umasikini kwani hapa awali tulikuwa tunaishi katika mazingira magumu hivyo kwa upande wetu tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa shirika la Plan international pamoja na Umoja wa ulaya amnbao ndio wamefadhuli mradi huu wa kuwawezesha vijana kiuchumi hasa sisi tuliokuwa katika hali dumu,”walisema.

Pia vijana hao walisema katika kufanikisha malengo ambayo wamejiwekea katika kufanya shighuli zao za ujasiriamali waliiomba serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kwamba inawasaidia katika kuwapatia mikopo na mitaji ambayo itaweza kuwaletea tija zaidi katika kukuza biashara zao na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Kwa upande wake Meneja ya mradi (YEE) wa kuwawezesha vijana kutoka Plan International Simon Ndembeche alisema kuwa mradi huo ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu una lengaa kuwasaidia vijana wanaoishi katika mazingira magumu ili kuweza kupata mafunzo ya kujifunza stadi mbali mbali ambazo zitawasaidia kujiajiri na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Naye Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo aliagiza halmashauri kuhakikisha fedha zote ambazo zinapatikana kupitia mapato ya ndani ziweze kuwanufaisha makundi ya vijana na wakinamama kwa lengo kuweza kuwasaidia katika shughuli zao za ujasiriamali ili kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi.

Jafo alisema kwamba mikakati ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawawezesha vijana na wakinamama katika suala zima la kiuchumi hivyo ili kuweza kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na wimbi la umasiniki.

MRADI huo ambao wa miaka mitatu umeanza kutekelezwa manamo mwaka 2015-2018 unasimamiwa na Shilika la Plan International kwa udadhili wa Umoja wa Ulaya umeweza kuwanufaisha vijana hao 592 ambao wameweza kupata fursa ya kufundishwa fani mbali mbali kutoka VETA, ikiwemo mapishi,mapambo, ushonaji, umeme wa majumbani,ufundi magari, pamoja na uchomeleaji vyuma,iseremala, pamoja na uedreva wa magari

No comments:

Post a Comment