Friday, February 2, 2018

MKURUGENZI MANISPAA YA DODOMA GODWIN KUNAMBI AKABIDHI VITAMBULISHO KWA MMACHINGA 140

Na Ramadhani Juma-Ofisi ya Mkurugenzi

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amekabidhi vitambulisho kwa Wafanyabiashara ndogo maarufu kama m Machinga wanaofanya shughuli zao katika soko la jioni ili waweze kufahamiana wakati wa biashara zao na hata kusaidia kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama.

Wafanyabiashara ndogo wapatao 140 wanaofanya shughuli zao katika eneo la Viwanja vya Nyerere wamekabidhiwa vitambulisho hivyo na Mkurugenzi huyo katika hafla fupi iliyofanywa katika viwanja hivyo mchana wa leo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Kunambi amewaasa wafanyabiashara hao kuwa na utamaduni wa kutunza akiba ili kukuza mitaji yao huku akiwaahidi kuwaboreshea mazingira ya kazi zao na kwamba hakuna kiongozi atakayewaondoa katika maeneo hayo mpaka watakapatiwa maeneo mbadala na rafiki kwa biashara zao.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli ni rafiki wa Machinga na ameshatoa maelekezo na nyinyi ni mashahidi…nawaahidi kusimamia maagizo ya Rais ya kuhakikisha wananchi wanyonge hawanyanyasiki ndani ya Nchi yao” alisema Kunambi.

Aliwataka wafanyabiashara kujiandaa kutumia fursa za ujenzi wa stendi mpya na ya kisasa na soko kubwa kwa ajili ya wafanyabiashara vitakavyojengwa katika Kata ya Nzuguni ili waweze kukua kibiashara.

“Tunaanza ujenzi wa stendi kubwa ya kisasa nay a mfano Afrika Mashariki na Kati katika eneo la Nzuguni Mwezi Machi 2018…ujenzi utakamilika baada ya miezi 24 na utaenda sambamba na ujenzi wa soko kubwa la kisasa kwahiyo jiandaeni kutumia hizo fursa” alisisitiz
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (wa pili kulia) akimvisha kitambulisho rasmi mmoja ya Wafanyabiashara ndogo wa soko la jioni katika eneo la viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara hao iliyofanywa leo Februari 2, 2018. Jumla ya Wafanyabiashara 140 wa eneo hilo wamepatiwa vitambulisho hivyo. Kulia ni Ofisa Masoko wa Manispaa hiyo Steven Maufi.
Baadhi ya Wafanyabiashara Ndogo wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akizungumza na Wafanyabiashara ndogo wa soko la jioni katika eneo la viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara hao iliyofanywa leo Februari 2, 2018. Jumla ya Wafanyabiashara 140 wa eneo hilo wamepatiwa vitambulisho hivyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (wa pili kulia) akimvisha kitambulisho rasmi mmoja ya Wafanyabiashara ndogo wa soko la jioni katika eneo la viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara hao iliyofanywa leo Februari 2, 2018. Jumla ya Wafanyabiashara 140 wa eneo hilo wamepatiwa vitambulisho hivyo. Kulia ni Ofisa Masoko wa Manispaa hiyo Steven Maufi.

No comments:

Post a Comment