MWENYEKITI
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dk.Titus Kamani amesema Serikali
kupitia tume hiyo ni awaelekeza viongozi wa Vyama vya Ushirika
kutojihusisha kuuza mali za vyama hivyo pasipo kuzingatia sheria.
Hivyo
amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika
kuuza mali za vyama hivyo na kufafanua ili kudhibiti hali hiyo Ofisi za
Mrajisi wa vyama vya ushirika imekuwa ikichukua hatua ikiwa pamoja na
kuwaondoa viongozi wanaokiuka sheria.
Dk.Kamani
amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anaelezea udhibito wa mali
za ushirika na mpango wa makusanyo na mauzo ya mazao makuu matano ya
kimkakati kupitia mfumo wa ushirika.
Amesema
vyama vya ushirika nchini vinaendeshwa kwa kuzingatia sheria ya vyama
vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013.Hivyo vyama vinapaswa kuzingatia
sheria wanapotekeleza majukumu yao.Dk.Kamani
amesema Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika inaelekeza
viongozi wa vyama hivyo kuwa makini kuzingatia sheria.
Amefafanua
vyama vina haki ya kumiliki mali na kuuza mali hizo pale itakapoona
inafaa kwa kuzingatia shetia iliyopo.Pia mali zinazomilikiwa na vyama
zinapaswa kuwa zimerasimishwa ili kuleta uhalali wa umiliki.
Dk.Kamani
amesema pamoja na uwepo wa taratibu za kisheria zinazoelekeza namna ya
ununuzi ,uuzaji na urasimishaji wa mali zake,baadhi ya viongozi wa vyama
wamekuwa hawazingatii na matokeo yake wamekuwa wakiingia kwenye
migogoro na wanaushirika.
Amesema
kutokana na uzito wa jambo hill la umiliki wa mali, mwaka 2016
akiwahutubia wananchi wa Jiji la Mwanza, Rais Dk.John Magufuli alieleza
jinsi viongozi wa vyama vya Ushirika wanavyohujumu vyama na
kujinufaisha.
Hivyo
alitoa maelekezo yakiwamo ya kurejeshwa kwa mali zote za vyama vya
vikuu vya Ushirika vya NCU (1984)Ltd na Shirecu (1984)Ltd zilizouzwa
kinyemela ambapo kutokana na agizo hill hadi sasa kati ya mali za NCU ,7
tayari zimerejeshwa na kati ya mali 2 za Shorecu zote zimerejeshwa .
"Kwa
dhati ya moyo wangu,nawashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa
nchi kwa imani kubwa waliyonayo juu ya Ushirika kwa kuutetea na
kuhakikisha unatumika kumkomboa mwananchi wa kipato cha chini," amesema
Dk.Kamani.Amesema
pia Serikali inawakumbusha wakurugenzi wa halmashauri za majiji
,manispaa ,wilaya na miji kuhakikisha vinakodi maghala kwa ajili ya
kuhifadhi pamba.
Hiyo
ikiwa ni maandalizi kwa vyama vya Ushirika katika msimu wa mwaka
2018/2019 kama yalivyo maelekezo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
No comments:
Post a Comment