Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema mara baada ya kuwasili nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018.
Marehemu Lulu Sylvester Mattunda Lema.
Familia katika picha ya pamoja eneo la Korogwe Bararara ya Tanga
Waombolezaji wakiwa nyumbani hapo
Sylvester Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo
Mwinjilisti wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza jambo baada ya mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema ulipowasili katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018 kwa taratibu za mazishi yanayofanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018 saa Nane Mchana, katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo, ambapo Lema alisema, "Katika mtihani huu ndugu yangu Sylvester,umeshinda katika ile ahadi uliyotamka ni kifo ndicho kitakacho tutenganisha mimi na wewe Lulu,hivyo ahadi hiyo umeitimiza, Profesa Lema pamoja na ndugu zako wote nachukua nafasi ya kuwapeni pole sana na Mungu akawatie nguvu, huyo aliyekufa maisha yake yamekwisha aliyebaki ndiye ameumia zaidi,wapo ndugu zetu waliokuwa Dar es Salaam ambao katika msiba huu walishughulika kufa kupona wahakikishe jambo hili limewezekana kama hivi lilivyowezekana, wapendwa niseme nivile tunauona msiba tukiusikia kwa mwingine, tumeona mwili umetufikia nyumbani,kutokana na msiba huu kuna watu wanashughulika kwa kujitolea kwa hali na mali, wapo wanaotoa matangazo wapo wanaofanya hili na lile kuhakikisha jambo linakwenda vizuri na wapo waliojitoa kwa hali na mali ,na kwa wale waliotoka Dar es Sallam na kwa wale waliotoka ndani na nje ya nchi naomba
kuwashukuru sana kwaniaba ya ushirika wa Nronga kwa kufanya juhudi zote kuuleta mwili wa mpendwa hapa nyumba pia napenda kuwaambia mumtie moyo ndugu yenu pamoja na watoto na mumtegemee Mungu Kwa mioyo yenu yote, huu mwaka ni mwaka wa marejesho, atarejesha amani
pasipo amani, atarejesha baraka pasipo baraka, atarejesha afya mahali afya imetoweka na huu mwaka nimzuri sana kwa anaemtegemea Mungu.
No comments:
Post a Comment