Saturday, January 6, 2018

MBUNGE MGIMWA:WATENDAJI KAMATENI WAZAZI WOTE AMBAO HAWAWAPELEKI WATOTO WAO SHULE

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi wa kata ya Kibengu kuhusu maswala mbalimbali ya kimaendeleo sambamba na kutoa maagizo mbalimbali ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya kata ya hiyo na jimbo hilo kwa ujumla
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa na viongozi wengine wakisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Kibengu
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akiangalia moja ya mradi wa ujenzi wa vyoo 
Diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi akiwa na viongozi wa kata ya hiyo mara baada ya kutoka kwenye kikao na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini


Na Fredy Mgunda,Mufindi. 


Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wote ambao hawataki kuwapele shule watoto wao wakifaulu mitihani ya shule ya msingi kwenda shule ya sekondari. 

Akizungumza na blog hii mbunge Mahamuod Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.

“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa

kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Ilogombe Pastor Haonga alisema kuwa wazazi wengi wa kata ya Kibengu wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Haonga

Haonga alimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kata ya Kibengu ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Haonga.

Aidha Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu

Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi
Nao watendaji wa vijiji vitano vya kata ya Kibengu ambao ni Dominicus Nyaulingo,Saifod Mwengwa,Haruna Kalenga, Richard Mandili na Demetus Kanyika walisema kuwa wamepokea agizo la mbunge na watalifanyia kazi kwa ukamilifu kwa kufuata sheria ili kuhakikisha watoto wa kata hiyo wanapata elimu kama inavyotakiwa.

Na kata ya Kibengu inajumuisha vijiji vitano ambavyo ni kijiji cha Kibengu,kijiji cha Igereke,kijiji cha Ilogombe,kijiji cha Usokami na kijiji cha Kipanga

No comments:

Post a Comment