Tuesday, January 9, 2018

DKT MASHINGO AHIMIZA NG'OMBE WENYE UMRI WA MIEZI SITA NA KUENDELEA KUPIGWA CHAPA



KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akiwaeleza na wafugaji wa Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma umuhimu wa zoezi la kupiga chapa ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.



Na Kumbuka Ndatta, KASULU

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo ameagiza ng’ombe wote wenye umri wa kuanzia miezi sita na kuendelea kuhakikisha wamepigwa chapa kabla ya kufikia tarehe ya mwisho ya upigaji chapa Januari 31 mwaka huu, kwani zoezi hilo sio la hiari bali ni la lazima na linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria.

Dk. Mashingo ametoa kauli hiyo wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa Wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.

Dk Mashingo aliwaambia wafugaji hao kutambua kuwa zoezi hilo linasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 na kuwasititiza kuwa haijulikani Serikali itaamua nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa hadi kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa ya Januari 31 mwaka huu.

Aidha Dk. Mashingo alitumia fursa hiyo kuwaelimisha wafugaji sehemu maalum ambayo ng’ombe anapotakiwa kupigwa chapa mwilini mwake ili kutoharibu ngozi yake inayotegemewa kwa matumizi mengine.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga amesema zoezi la upigaji chapa linaendelea vizuri na mwitikio ni mkubwa kutoka kwa wafugaji ambapo jumla ya ng'ombe 93,182 wameshapigwa chapa kati ya ng'ombe 345,469 waliotambuliwa ambao ni sawa na asilimia 27.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Fatima Laay amemweleza Katibu mkuu kuwa jumla ya ng'ombe 7,552 kati ya 10,000 wenye umri wa zaidi ya miezi sita na kuendelea tayari wameshapigwa chapa ambao ni sawa na asilimia 75.52.

Kwa upande wake Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko alikiri kuwepo tatizo la Ng'ombe kupata vidonda vikubwa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo jambo lilochangiwa na wafugaji kutoelimishwa sehemu sahihi ya kupiga chapa mifugo.

"Mimi ng'ombe wangu bado hawajapigwa chapa,waliopigwa chapa walipata vidonda vikubwa kwa hiyo kama wataalam wetu ngazi ya vijiji wameelimishwa vizuri jinsi ya kupiga chapa basi haina shida nitawapeleka ng'ombe wangu wakapigwe chapa na kuhamasisha wananchi wengine kuunga mkono zoezi hili "alisema Nsanzugwanko.

No comments:

Post a Comment