Tuesday, January 2, 2018

DK. MNDOLWA AKABIDHIWA RASMI OFISI LEO, AAHIDI KUUNDA KAMATI KUTAFUTA UFUMBUZI DHIDI YA KUMOMONYOKA KWA MAADILI KATIKA JAMII YA KITANZANIA

 Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar  Abdallah Haj Haidar.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Seif Shabani Mohamed alipowasili Makamo Makuu ya Jumuiya hiyo kwa ajili ya makabidhiano hayo
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa  akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Najma Giga wakati wa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Mndolwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Makamu Menyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Abdallah Haj Haidar
 Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wqzazi Tanzania Abdallah Bulembo akionyesha Katiba ya Jumuiya hiyo kabla ya Kumkabidhi Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hizo Zanzibar Abdallah Haj Haidar
 Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo, kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani Mohammed na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar  Abdallah Haj Haidar. 
 Bulembo akiendelea kukabidhi nyaraka
 Dk. Mndolwa na Bulembo wakisaini nyaraka za makabidhiano
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania  Zanzibar  Abdallah Haj Haidar na Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani Mohammed wakisaini nyaraka upande wa mashahidi
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Edmund Mndolwa akizungumza baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi
 Dk Mndolwa na Bulembo wakifurahia jambo baada ya makabidhiano ya ofisi
Watumishi wa Jumuiya ya Wazazi Makao Makuu wakiwa kazini wakati wa makabidhiano hayo ya ofisi baina ya Dk Mndolwa na Bulembo PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Na Bashir Nkoromo.

Mwenyekiti mpya wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuunda Kamati ya  kutathmini namna Jumuiya hiyo inakavyolishughulia kwa ufanisi tatizo la kuporomoka kwa maadili katika jamii hapa nchini.

Dk. Mndolwa ametoa ahadi hiyo leo, hayo wakati akikabidhiwa rasmi Ofisi na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo, hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania jijini Dar es Salaam.

"Katika hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli alitutaka sisi viongozi wa Jumuiya hii tusikae kimya wakati vitendo vya kuporomoka kwa maadili katika jamii ikiwemo wasanii wa kike kuonyesha sehemu za miili yao zinazotakiwa kusitiriwa. Sasa hili ni agizo lazima mimi na viongozi wenzangu tulipe kipaumbele katika kulifanyika kazi.

Kwa hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi leo hii, miongoni mwa mipango yangu Kama Mwenyekiti ni Kuunda Kamati itakayojikita kwa undani kuhakikisha tunapata njia bora za kudhibiti kuporomoka kwa maadili katika jamii ya Watanzania", alisema Dk Mndoldwa. Alisema, pia atahakikisha katika zama za uongozi wake, Jumuiya ya Wazazi inainuka na kujitegemea vya kutosha kiuchumi ili iondokane na adha ya kuwa ombaomba.

"Jumuiya hii ianazo mali nyingi, kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha fedha zinazotokana na mali au miradi hii zinaingia kwenye hazina ya Jumuia badala ya kupotelea mifukoni mwa wajanja wachache, tukifanikiwa kuthibiti bila shaka tutakuwa na fedha za kutosha", alisema Dk. Mndolwa.

Akimzungumzia Bulembo, Dk Mndolwa amesema, alikuwa kiongozi bora ambaye ameisaidia kwa kiasi kikubwa Jumuiya ya Wazazi, na kwamba katika jitihada zake ameiboresha Jumuia hiyo kwa karibu asilimia tisini.

"Nimejifunza mambo mengi kwa Bulembo, mojawapo ni uvumilivu, huyu ni mvumilivu kiasi kwamba itanibidi kuiga uvumilivu wake ili na mimi nistaafu kwenye Jumuiya hii nikiwa safi kama yeye," Alisema Dk. Mndolwa.

Kwa Upande wake Bulembo aliwataka viongozi wapya wa Jumuiya hiyo kuthamini sana Waaandishi wa habari kwa kuwapa ushirikiano kila unapohitajika na kwamba yupo tayari kutoa ushauri pale utakapohitaji.

Aliwaasa viongozi wapya kuendeleza mazuri yaliyofanywa na uongozi uliopita huku wakiachana na mabaya yaliyofanyika wakati huo.

"Namna nzuri ya kuongoza ni kuwa karibu na unaowaongoza, msikae nao mbali mnaowaongoza na ikiwa kutakuwa na jambo miongozi mwenu viongozi ambalo haliendendi vizuri utatuzi wake uwe kwenye vikao si kwingineko", Alisema Bulembo.

No comments:

Post a Comment