Wednesday, December 6, 2017

WATAALAM SEKTA YA MADINI WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO GGM

Wataalam kutoka Taasisi za Serikali zinazohusika na Sekta ya Madini ndani na nje ya nchi pamoja na Wakufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Mkufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI), Colleen Crystal (kulia) akizungumza na wataalam wa Madini wa Tanzania na nje ya Tanzania wakati walipofanya ziara ya mafunzo katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) .
Wataalam wa Madini wa Tanzania na nje ya nchi wakiangalia eneo ambalo uoteshaji wa miti umefanyika baada ya uchimbaji madini kukamilika lengo likiwa ni kuhifadhi mazingira mara baada ya shughuli za uchimbaji madini kukamilika katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) .
Mkufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI), Colleen Crystal (kushoto) akizungumza na Wataalam wa Madini wa Tanzania na nje ya Tanzania wakati walipofanya ziara ya mafunzo katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) .
Wataalam wa Madini wa Tanzania na nje ya Tanzania wakiangalia shughuli za uchimbaji madini katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika Mgodi huo.
Sehemu ya eneo linalotumika kuhifadhi mabaki ya uchenjuaji (tailings) katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) ili mabaki hayo yasiweze kuleta madhara kwa binadamu na mazingira kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment