Thursday, December 21, 2017

SHAKA ATEMA NYONGO,ASEMA YUPO TAYARI KUWAJIBA IWAPO KUNA UFISADI

Na Said Mwishehe,blogu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)Shaka Hamdu Shaka amesema yupo tayari kuwajibika iwaoi itabainika anefanya ufisaidi wa aina yoyote katika utendaji wake kwenye nafasi aliyonayo sasa.

Shaka ametoa kauli hiyo kwenye ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni jijini Dar es Salaam leo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa Kheir James Denis ambaye amepokelewa rasmi na kutambulishwa kwa vijana wa mkoa huo.

Amesema katika nafasi hiyo amekuwa akifanya jitihada mbalimbali za kutetea mali za umoja huo na kwa bahati mbaya hatua hiyo imemfanya apigwe vita na kumkwamisha.Amesema chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,Dk.John Magufuli ataendelea kusimama imara kusimamia rasilimali za umoja huo na hatarudi nyuma.

Amesema amekuwa katika mazingira magumu yanayotokana na kupigwa na ikafika mahali baadhi ya watu wakaanza kumzushia mambo ambayo hayana ukweli wowote.Ametumia nafasi kueleza wazi yupo tayari kuchunguzwa na kuwa tayari kuwajibika iwapo itabainika ameshiriki kufuja mali za umoja huo."Nimeshambuliwa na kupigwa vita kwasababu tu ya kuwa na msimamo thabiti wa kusimamia mali za jumuiya na maadili.

" Naomba niseme leo hii ni siku ya historia kwangu kwani nimetoa la moyoni ambalo nimekuwa nalo muda mrefu,nimeshambuliwa na kupigwa vita bila sababu.Niseme nipo tayari kuwajibika kama nitabainika kufanya ufisadi kwa kutumia bafasi yangu,"amesema Shaka.

Amesema katika kusimamia mali za umoja huo amebaini kuliwa kwa zaidi ya Sh milioni 250 katika mabanda ya maduka ya biashara eneo la Ukumbi wa Vija a Social Hall Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema kuliwa fedha hizo wakaamua kusimamisha shughuli za kibiashara na kinachoendelea kwa sasa ni kubomoa eneo hilo na kujengwa jengo la kitega uchumi ambalo litaingizia fedha umoja huo.

Ameelezea namna ambavyo amekuwa akitiwa moyo na Rais Magufuli na kufafanua hatarudi nyuma atashirikiana na mwenyekiti wa umoja huo taifa kuusimamia umoja huo.

No comments:

Post a Comment