Wednesday, December 6, 2017

SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA HUDUMA ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imezindua mwongozo wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya tiba ikiwemo zahanati, vituo vya afya na hospitali ikiwa ni katika kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya  kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iitwayo NIPO TAYARI.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Sekta Ofisi ya Rais Tamisemi, Dkt. Andrew Komba amesema uzinduzi wa mwongozo huo ni katika kueleka awamu ya pili ya kampeni ya NIPO TAYARI itakayozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais,Mhe. Samia Suluhu Hassan ifikapo Desemba 7 mjini Dodoma.

“Mwongozo huo utasimamia na kutekeleza shughuli zinazohusiana na mazingira na umelenga katika kutoa maelezo stahiki namna ambavyo vituo vya afya, ikiwemo ngazi za chini mpaka juu ili maelekezo hayo yaweze kutumika katika upangaji wa mipango na uandaaji wa bajeti zitakazotumika,” amesema Dkt. Komba. Aidha Dkt. Komba amesema kuwa watanzania tunatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira pamoja kutumia vyoo bora ili kuweza kudumisha afya njema kwa maendeleo ya Tanzania.

Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi ya Mazingira, Anyitike Mwakitalima amesema kuwa kampeni hiyo inalenga kuwahamisha wananchi kuweza kutumia vyoo bora na mpaka kufikia Juni 2021 kaya zote nchini ziwe zinatumia vyoo. “Kutokana  na kulegalega  katika baadhi ya maeneo, waligundua kwamba kisababishi kimojawapo ilikuwa ni ukosefu wa mwongozo wa taifa ambao wadau na serikali ingeutumia kusimamia usafi wa mazingira kwahyo kampeni hii itahakikisha mpaka kufikia 2025 kaya zote zinatumia vyoo vilivyo bora” alisema Bw. Anyitike.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango kutoka Shirika la Water Aid, Abel Duganga amesema kutokana na kukosekana kwa mwongozo huo unaopima hali ya maji nchini utendaji wa serikali na wadau ulikuwa ukisuasua,  lakini sasa utawezesha kuwa na vigezo vinavyofanana katika kupima na kuwa na takwimu sahihi.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha usafi wa Mazingira Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Stephen Kiberiti akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Andrew Komba wa pili kutoka kushoto katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya.
Wadau wa masuala ya Afya na Usafi wa mazingira wakifuatilia kwa ukaribu taarifa kutoka kwa mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mipango WATERAN Tanzania Abel Dugango akisoma taarifa fupi kuhusu huduma za maji na usafi wa mazingira mbele ya Viongozi wa Wizara na Wadau wa Sekta ya Afya, shughuli inayoendelea jijini Dodoma.
Mratibu wa Kampeni ya kitaifa ya Usafi na Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Anyitike Mwakitalima akitoa taarifa fupi mbele ya wadau wa Afya katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Mkutano wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya kulia ni mmoja wa waratibu wa kampeni ya Usafi wa Mazingira.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Bumi Mwamasage akipokea mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira kutoka kwa Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dr. Andrew Komba ambae pia alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akipokea vipeperushi vilivyoandaliwa kwaajili ya kutoa elimu kutoka kwa Salome Mtenga.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba akiwa na Wadau wa masuala ya Afya katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment