Thursday, December 7, 2017

Jaffo:Stawavumilia wakurugenzi na wenyeviti wa kamati za fedha ambao hawatatoa fedha za maendeleo


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo amesema hatawavumilia wakurugenzi na wenyeviti wa kamati za fedha ambao hawatatoa fedha za maendeleo zinazotokana na mapato ya ndani ya halmashauri kulingana na bajeti zao.

Alitoa onyo hilo wakati akifungua kongamano la siku mbili la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

Jafo alisema wakurugenzi na wenyeviti hao wataondolewa katika nafasi zao endapo watashindwa kutoa fedha hizo ikiwa ni pamoja na asilimia tano za mapato ya ndani kwa vikundi vya vijana na wanawake.

“Wakarugenzi watakaoshindwa kutoa fedha katika mapato yao ya ndani hawatatosha katika kipindi cha utawala huu, umeipanga katika bajeti , umekusanya halafu vijana na akina mama hujawapelekea asilimia tano za mapato ya ndani, basi mkurugenzi utakuwa hutoshi”

Jafo pia alitaka Bodi za mikopo katika kila halmashauri kuhakikisha wanatoa mikopo kwa kulenga viwanda ili kusukuma agenda ya uchumi wa kati.Aidha, Jafo aliiomba taasisi ya WAJIBU kuja na kongamano la mafunzo kwa madiwani na kamati za fedha kote nchini kupewa mafunzo kama hayo ili isaidie kusukuma agenda ya viwanda.

“Madiwani wengi bado wanachangamoto kubwa, mkiwaelemisha madiwani na kamati za fedha itasaidia agenda hii ya viwanda, tutapata watu ambao wanawajibika na wanafanya kile wanachokielewa, ninyi WAJIBU ni wabobezi kwenye usimamizi wa fedha.”

Alisema agenda ya serikali ya Tanzania ya viwanda imetokana na mtazamo wa wananchi wa kutaka mabadiliko na kuwa rais John Magufuli ametafsiri ili kufikia agenda hiyo ni kwa viongozi kufanya uthubutu wa kuamuani na kuongeza kuwa tayari serikali inaendesha miradi mikubwa mitatu ya kuboresha miundombinu ili kuwafikia hata walioko vijijini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh alisema Mamlaka za serikali za mitaa ni muhimu katika kaendeleo na na pia zina nafasikubwa kusukuma mebele agenda ya uchumi wa kati kupitia viwanda.

“ Naamini kama viongozi wataacha kufanya kazi kwa mazoea na kufuata kasi ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli basi viongozi wataweza kusaidia maendeleo na kuacha alama,”Aidha, Utouh alisema taasisi yake iko mbioni kuandaa mfumo ambao utasaidia kufanya tathimini ya kisayansi ya utendaji na uwajibikaji wa viongozi wa serikali za mitaa.
 .WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo akizungumza katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtenda wa Wajibu, Lodovick Utouh akizungumza juu madhumuni ya mkutano huo kwa wenyeviti wa halmashauri, Mameya na Wakurugenzi juu ya upangaji mikakati ya kuhudumia wananchi katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Wajibu, Yona Kilaghane akizungumza juu maazimizio na utekelezaji wa wajibu maombi ya WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu, Hadson Kamoga akizungumza na waandishi wa habari juu utekelezaji wa maazimio yatakayotokana na kongamano hilo katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
 Sehemu wenyeviti wa halmashauri, Mameya na Wakurugenzi
picha ya pamoja ya Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo pamoja Wenyeviti wa halmashauri, Mameya na Wakurugenzi


No comments:

Post a Comment